Monday, August 24, 2015

” Kuna tofauti kubwa kati ya Ndanda na Stand United” – Jacob Masawe
Jacob Masawe amefurahishwa na mambo mengi katika timu hiyo huku akikiri wazi kuwa maisha ni tofauti na yale yaliyokuwepo Ndanda FC

Mshambulizi mpya wa klabu ya Stand United, Jacob Masawe amefurahishwa na mambo mengi katika timu hiyo huku akikiri wazi kuwa maisha ni tofauti na yale yaliyokuwepo Ndanda FC ambayo aliichezea gemu 27 na kufunga jumla ya magoli 7 msimu uliopita.
” Kuna tofauti kubwa kati ya Ndanda na Stand. Kuanzia kwenye benchi la ufundi, udhamini hata kwa wachezaji. Walio wengi ni wenye uzoefu mkubwa wa ligi” anasema mchezaji huyo mwenyeji wa Shinyanga wakati alipozungumza na Goal.
Hamad Kakut Ndikumana, Nassoro Chollo, Hussein Javu ni baadhi ya wachezaji wapya walioungana na Mkufunzi, Mfaransa, Patrick Liewig kama maingizo mapya yenye uzoefu katika timu.
” Tayari nimekutana na vitu vipya kutoka kwa mwalimu, Liewig. Hakika anajua sana kufundisha mpira”. Kitendo cha Masawe kuichagua Stand na kuzitosa baadhi ya timu zilizokuwa zikimuwania kimewavutia wapenzi wengi wa kandanda mkoani, Shinyanga kwa kuamini sasa wamepata ‘mwokozi’ ambaye ni ‘mtoto wa nyumbani’.
” Wachezaji wote wapya wamepokelewa vizuri. Kwa upande wangu, mashabiki wamefurahishwa sana na kujiunga kwangu katika timu hii. Kwao, mimi ni kama mfalme wao. Sitawaangusha nitajitahidi kushirikiana na wenzangu katika timu ili kuipaisha Stand.”

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe