
Hawa ni wachezaji wa Simba wakuchungwa kwenye kikosi
cha Simba cha 2015/16 wanaohitaji ulinzi mkali vinginevyo wanaweza
kuhatarisha vibarua vya makocha wa timu pinzani
ZIMEBAKI wiki chache kabla ya msimu mpya wa Ligi ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16 kuanza kutimua vumbi huku timu 16 zikiwania taji hilo ambalo kwa sasa linashikiliwa na klabu ya Yanga ambayopia ndiyo bingwa wa kihistoria kwa kuchukua ubingwa huo mara 25.
Timu hizo za Ligi Kuu na zile za Daraja la kwanza hivyo bila shaka klabu nyingi kwa asilimia kubwa zitakuwa zimekamilisha usajili wao na kama bado basi zipo katika hatua za mwisho kufanya hivyo.
Niwazi kila kocha atakuwa ametuliza kichwa chake na kufanya usajili mzuri wa kukiimarisha kikosi chake kwa lengo la kupata matokeo mazuri katika ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali hasa baada ya Shirikisho la soka Tanzania kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka watano hadi saba.
Ifuatayo ni orodha fupi ya wachezaji wa Simba ambayo imeandaliwa na Mtandao wa Goal ikianisha wachezaji wakuchungwa kwenye kikosi cha Simba cha 2015/16 wanaohitaji ulinzi mkali vinginevyo wanaweza kuhatarisha vibarua vya makocha wa timu pinzani.
1.Hamisi Kiiza ‘Diego’
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambaye msimu huu amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kucheka na nyavu alivyokuwa Yanga na hata timu yake ya taifa The Cranes ya Uganda.
Kiiza anatarajiwa kufanya makubwa msimu uhao kwenye ligi ya Vodacom ambayo inataraji kuanza Septemba 12 kutokana na uwezo aliokuwa nao lakini hata viungo wanaomchezesha akina Jonas Mkude na Said ndemla.
Kiiza amekuwa hatari sana anapokuwa kwenye eneo la hatari la timu pinzania na mshambuliaji huyo amekuwa akiwasumbua sana mabeki kwani mara wamekuwa hawamuoni na pindi anapoonekana basi anakuwa anashangilia kwenye kibendera .
2.Ibrahim Ajibu
Mshambuliaji anayechipukia kwa kasi kwenye kikosi cha Simba na alidhihirisha uwezo wake msimu uliopita chini ya kocha Goran Kopunovic kwa kufunga mabao sita huku ikiwa ndiyo msimu wake wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Ajibu ameonyesha kuwa yeye ni mchezaji hatari anapokuwa kwenye lango la timu pinzani na ndiyo maana kocha mpya wa Simba Dylan Kerr, amemchagua kuwa mshambuliaji wa kwanza atakayeshirikiana kwa karibu ama na Mussa Hassan ‘Mgosi au Kiiza.
Uwezo aliouonyesha Ajibu msimu uliopita msimu huu anatarajiwa kufanya mambo makubwa zaidi na anakadiriwa kufunga mabao zaidi ya 10 kutokana na kiwango alichokuwa nacho.
3.Mussa Hassan ‘Mgosi’
Amerudi nyumbani kwa mara ya pili baada ya kuondoka misimu mitatu iliyopita akitimkia DC Motema Pembe ya DR Congo , JKT Ruvu na msimu uliopita alicheza Mtibwa Sugar ya Morogoro
Hakuna asiyejua uwezo wa Mgosi, aliyewahi kuwa mfungaji bora kwenye msimu wa 2009/10 akiwa na Simba kurudi kwake kumerudisha matumaini ya mashabiki wa timu hiyo kuwa wanaweza kuchukua ubingwa msimu ujao.
Mgosi aliifungia Mtibwa Sugar mabao 7 msimu uliopita na kuonyesha yeye ni moto wa kuotea mbali ndiyo sababu ya Simba kuamua kumrudisha kundini ili aweze kuongeza nguvu akishirikiana na Kiiza na Ajibu ili kutimiza malengo yao ya ubingwa.
4.Said Ndemla
KIUNGO mchezeshaji anayesemekana kuwa na mapafu ya Mbwa anasifika na uwezo mkubwa wa kutuliza presha ya timu na kupiga pasi za mwisho lakini hata kufunga kwa mashuti makali anapokuwa nje ya 18 ya timu pinzani.
Ndemla alifanya vizuri sana msimu uliopita na kufunga mabao mawili kitu ambacho kiliulazimu uongozi wa Simba kumuongezea mkataba wa miaka miwili kwa ofa ya Sh. 30 milioni ili kuendelea kupata huduma yake msimu ujao.
Tayari kocha mpya Dylan Kerr, amemteua mchezaji huyo kama kamanda mkuu kwenye safu ya kiungo licha ya ujio wa Mwinyi Kazimoto hiyo inatokana na kuvutiwa na uchezaji wake ambao kama asipo chungwa vizuri na wachezaji wa timu pinzani au kupata majeruhi anatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali na kuipa mafanikio timu yake.
5.Laudit Mavugo
Mshambuliaji mpya anayetarajiwa kutua wakati wowote kwenye klabu ya Simba ambaye anatajwa kuziba pengo la Mganda Emmanuel Okwi aliyeuzwa Denmark wiki mbili zilizopita.
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi anatarajiwa kuwa na madhara makubwa kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kupachika mabao kuthibitisha hilo wiki iliyopita ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi ya Burundi kutokana na mchango aliotoa kwa timu yake ya Vital O’.
Uongozi wa Simba kwa sasa unapigana kuhakikisha unatumia vizuri sikuzilizobaki ili kuhakikisha zinaipata saini ya mshambuliaji huyo mwenye kila sifa ya kuweza kurudisha heshima ya klabu hiyo ambayo imepotea kwa misimu mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment