Monday, August 24, 2015

Papa Niang atua kumalizana na Simba, huku Kimwaga akisaini mwaka mmoja
Kimwaga amekwenda Simba kwa mkopo baada ya kukosa nafasi katika kikosi chake

STRAIKA Papa Niang raia wa Senegal ametua nchini tayari kwa mazungumzo ya mwisho ya usajili na timu ya Simba huku Wekundu hao wa Msimbazi wakimpa mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji wa Azam, Joseph Kimwaga.
Kimwaga amekwenda Simba kwa mkopo baada ya kukosa nafasi katika kikosi chake kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu tangu alipopata majeraha ya goti lake msimu wa 2013/14.
Kimwaga amepewa mkataba huo baada ya kufanyiwa vipimo vya afya jana ambapo viongozi wa Simba waliridhishwa na majibu ya vipimo hivyo na sasa atajiunga na kikosi hicho cha Dylan Kerr.
Viongozi wa Simba wamekiri juu ya usajili huo na kwamba wana imani kubwa na mshambuliaji huyo kutokana na kipaji alichonacho "Tumempa mkataba wa mwaka mmoja na tumejiridhisha juu ya afya yake

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe