Monday, June 23, 2014


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangara na Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Bw. Li Jinzao wakitia saini Mikataba ya Muendelezo wa awamu ya Tatu ya Ujenzi wa Uwanja wa Taifa pamoja na Makabidhiano ya gari la kurushia matangazo (OB VAN)  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangara na Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Bw. Li Jinzao wakibadilishana Hati ya Makubaliano wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mukangara wakifurahia  jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Abdalah Kigoda wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimkaribisha Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Dorothy Mwanyika na Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Bw. Li Jinzao wakitia saini Mkataba wa kusaidia Mafunzo ya Riadha Nchini wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Dorothy Mwanyika na Waziri wa Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Bw. Li Jinzao wakibadilishana Hati ya Makubaliano wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimueleza jambo Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao mara baada ya hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete mara baada ya hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiteta jamabo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na Tanzania leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe