Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeandaa gulio kubwa la wazi kwa ajili ya mauzo ya bidhaa mbalimbali za simu, ipad na bidhaa nyengine zinazofanana na hioz kwa lengo la kuwakwezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kupata simu hizo kwa gharama nafuu zaidi ya gharama za kawaida za sokoni.
Gulio hilo maarufu kwa jina la Vodacom Expo
ni la pili kuandaliw ana Vodacom na linatarajiwa kufanyika kwa siku
mbili mfululizo kuanzia tarehe 28 na 29 mwezi huu katika viwanja vya
Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo,
Salum Mwalim amebainisha kuwa Vodacom Expo ni tukio kubwa ambalo wateja
wa Vodacom na watanzania kwa ujumla hupata fursa ya kununua simu za
kisasa na bidhaa za mawasiliano zenye ubora kwa bei ya chini tofauti na
wanazouziwa madukani.
"Mwaka jana kwa mara ya kwanza tulipoitisha
gulio hili tulishuhudia idadi kubwa ya watu wakifurika kwa ajili ya
kupata bidhaa mbalimbali za simu za mkononi, hali hiyo ilitupatia ujumbe
kuwa wazo tulilolibuni limepokelewa vema na watanzania na kwmaba ipo
haja ya kurudio tena tukio hilo ili tuwapatie tena fursa ya kupata simu
za aina mbalimbali kwa gharama nafuu zaidi."
Mwalim amesema uamuzi wa kufanya gulio hilo
katika viwanja vya Leaders ni kuweza kukabiliana na changamoto ya
msongamano wa watu kufuatia idadi kubwa ya watu wlaiohudhuria gulio la
mwaka jana.
Akizungumzia baadhi zitakazopatikana siku
hiyo, Mwalim amesema "Safari hii simu za kisasa zikiwemo za smartphone
ni nyingi zaidi kutoka makampuni tofauti na kizuri zaidi zitakuwa
zimeunganishwa na ofa za vifurushi mbali mbali kutoka Vodacom kama vile
muda wa maongezi, sms na intaneti."
Aliongeza
Mwalim amesema kuw lengo la Vodacom ni kutaka kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uwezo wa kumiliki simu bora na ya kisasa kwa ajili ya mawasiliano ya sauti na huduma za intanenti ili kuendana na aksi ya maendeleo kwenye huduma za simu za mkononi ambayo Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayoendelea.
Mwalim amesema kuw lengo la Vodacom ni kutaka kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uwezo wa kumiliki simu bora na ya kisasa kwa ajili ya mawasiliano ya sauti na huduma za intanenti ili kuendana na aksi ya maendeleo kwenye huduma za simu za mkononi ambayo Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayoendelea.
"Kupitia mtandao wetu tunajitahidi kadri ya
uwezo wetu kumuwezesha kila mtanzania kumudu kumilki smartphone.
Ningependa kuwaondoa shaka wateja wetu kuwa safari hii bidhaa ni nyingi,
bei nafuu, muda wa manunuzi umeongezwa zaidi na hii yote ni kutokana na
maoni tuliyoyapokea kutoka kwenu na kuyafanyia kazi, naomba mjitokeze
kwa wingi siku hiyo."Aliongeza Mwalim.
0 comments:
Post a Comment