
STAA wa Shindano la Maisha Plus ambaye sasa ni muigizaji, Upendo Mushi ‘Pendo’ ameshindwa kuzuia hisia zake za kimapendo na kufunguka kuwa anampenda sana mwimbaji Kalala Junior.

Staa wa Shindano la Maisha Plus ambaye sasa ni muigizaji, Upendo Mushi ‘Pendo’
Akitema stori mbili tatu na paparazi wetu katika msiba wa dairekta
George Tyson baada ya kumuona Kalala kwa mbali, Pendo pasipo kufafanua
kwa undani, alisema anampenda kuliko maelezo nyota huyo wa muziki wa
dansi.“Jamani niwe mkweli tu, nampenda sana Kalala tuweke utani pembeni na mwenyewe anajua sababu nilishawahi kumwambia,” alisema Pendo.
Risasi linaendelea kuwachimba wawili hao, mzigo ukikaa sawa, tutawajuza.
0 comments:
Post a Comment