
KOCHA wa Mbeya City, Juma Mwambusi ameona wachezaji kadhaa wa
kigeni kwenye michuano ya Mto Nile lakini haruhusiwi kuwasajili kutokana
na sera za klabu hiyo.
Alisema sera na uongozi wa timu yake unataka kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania na siyo kuwapapatikia wachezaji wa nje.
“Niliwaona vijana wengi Sudan wenye vipaji vya
hali ya juu na nilitamani wachezee Mbeya City, lakini malengo ya timu ni
kutaka kuinua vipaji vya vijana wa kitaifa hususan wa Jiji la Mbeya na
siyo wachezaji wa kimataifa,” alisema.
Alisema akiwa Sudan aliishia kumezea mate
wachezaji wazuri. ‘’Tunasubiri Juni 15 mwaka huu ambapo tutatangaza
usajili mpya wa kikosi chetu, hivyo mashabiki na wapenzi wa Mbeya City
wawe na imani na kikosi kitakachotangazwa kwa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment