
David Moyes
KWELI Manchester United iliingia mkenge kwa David Moyes baada ya kila kitu alichokifanya klabu hapo kugeuka kuwa majanga.
Baada ya kocha huyo kuisababisha hasara kubwa ya
kupoteza mamilioni ya pesa kutokana na kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa
Ulaya miamba hiyo ya Old Trafford itapata hasara kubwa kwa kiungo wao
Marouane Fellaini, ambaye alisajiliwa na kocha huyo.
Kocha Mkuu mpya wa kikosi hicho, Louis van Gaal
amesema haoni kama kiungo huyo anaweza kupata nafasi kwenye timu hiyo
msimu ujao na kwamba yupo sokoni kwa pauni 15 milioni kitu ambacho
kitaifanya Man United kuingia hasara ya pauni 12.5 milioni.
Fellaini alinunuliwa na Moyes mwaka jana kwa ada
ya pauni 27.5 milioni, lakini kwa msimu mzima aliocheza kwenye kikosi
hicho cha Man United hakufunga bao hata moja kitendo kinachomfanya kocha
mpya, Van Gaal afichue bayana kwamba atakapoingia Old Trafford basi
hamtaki mchezaji huyo.
Kiungo huyo Mbelgiji kwa sasa yupo kwenye fainali
za Kombe la Dunia na kikosi cha Ubelgiji nchini Brazil na kitu kipekee
kitakachomfanya aendelee kubaki Old Trafford msimu ujao kama atafanya
kweli kwenye fainali hizo.
Hata hivyo, licha ya Man United kukubali kumuuza
kwa hasara, hakuna klabu yoyote iliyojitokeza kutaka kumsajili kiungo
huyo kitendo kijachothibitisha kwamba mzigo huo bado unaikabili timu
hiyo.
0 comments:
Post a Comment