
SIMBA inanunua wachezaji wawili tu wapya wa kigeni, lakini bajeti yake ya usajili mzima wa kikosi ni Sh300 milioni.
Fungu hilo limetengwa na kundi maarufu la Friends
of Simba ambalo Mwanaspoti linajua kwamba wanamsapoti Evans Aveva kwenye
nafasi ya urais katika uchaguzi ujao wa Juni 29.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba
kundi hilo limefanya kikao na watu wa Kamati ya Usajili na kutenga
bajeti hiyo ingawa baadhi wanadhani inaweza kupungua kufikia
Sh250milioni.
Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, alisema kiasi hicho
cha fedha kitakuwa maalumu kwa ajili ya malipo ya wachezaji
watakaosajiliwa sasa na wale wanaoidai klabu hiyo baada ya kubainika
kuwa benchi la ufundi limependekeza baadhi ya mikataba ya wachezaji
isitishwe.
“Tunaamini kiasi hicho kitatosha kabisa bila
matatizo kututafutia wachezaji halisi ambao watarudisha heshima ya
Simba, unajua watu wana uchungu na Simba yao,” alisema bosi huyo.
“Endapo Michael Wambura atarudishwa katika mbio za uchaguzi, basi ni
wazi suala la kusajili litachelewa zaidi mpaka hapo uchaguzi
utakapomalizika, lakini wakimwondoa nakuhakikishia baada ya wiki moja
tutaanza kusajili rasm
0 comments:
Post a Comment