Man United yaweka mezani mamilioni kumnasa Robben

Supastaa wa Bayern Munich, Arjen Robben.
MANCHESTER United imeripotiwa kuweka mezani kiasi cha Pauni 40 milioni ili kumnasa supastaa wa Bayern Munich, Arjen Robben.
Taarifa ya kutoka kwa mtu wa karibu wa kocha Louis
Van Gaal alisema kwamba anaamini winga huyo mwenye umri wa miaka 30
atakuwa mchezaji muhimu sana kwake wakati atakapoanza kibarua chake Man
United msimu ujao.
Robben kwa mara ya kwanza alinunuliwa na Van Gaal
alipokuwa akiinoa Bayern Munich na baada ya kufanya kazi pamoja kwenye
kikosi cha Uholanzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Mdachi huyo
anaamini kwa kiasi hicho cha pesa kilichowekwa mezani kitawashawishi
Bayern na kukubali kufanya biashara.
Mwezi uliopita, Robben alikaririwa akiondoa
uwezekano wa yeye kuhamia Man United huku akimalizia kwa kusema kwamba
kama Bayern watakubali kumuuza basi hawezi kupinga jambo hilo.
Robben alisema amekuwa na furaha Bayern, lakini
maisha ya soka yamekuwa yakibadilika kila kukicha kitu ambacho kinaweza
kutokea na hivyo msimu ujao akawa ndani ya jezi za Man United.
0 comments:
Post a Comment