
JAMBO limezua jambo! Katika hali ya kushangaza, mgeni rasmi katika shughuli ya kumbukumbu cha kifo cha aliyekuwa staa wa muziki wa Hip Hop Bongo, Albert Mangwea ‘Ngwea’ amejikuta akichafua hali ya hewa.

Ilielezwa kuwa, Abood aliyekuwa na majukumu mengine, alishindwa kufika hivyo kumtuma katibu wake, Mourice Masala ambaye alichafua hali ya hewa kwa kusema wasanii wasikubali kutumiwa na wanasiasa wala wasikubali kubebeshwa mizigo na matajiri.
Mbali na kauli hiyo, mwakilishi huyo akaenda mbele zaidi kwa kuwataka wasanii waachane na skendo mbaya kwani kila kukicha jamii imekuwa ikisikia mabaya yao. Hapo ndipo umati uliokuwemo ukumbini humo sanjari na ndugu wa marehemu ukaibua miguno ya mshangao wengine wakihoji mgeni huyo alikuwa akimaanisha nini kusema hivyo!
“Mh! Sasa huyu mgeni inakuwaje anaanza kuwananga wasanii wasikubali kuwa punda? Kwani nani alikuwa punda? Anataka kutwambia marehemu (Ngwea) alikuwa punda? Anatuzingua huyu naye,” alisikika mmoja wa waalikwa.
Punda ni mtu anayebebeshwa mzigo wa madawa ya kulevya ‘unga’ kwenda kuuza kwingine.
Minong’ono hiyo ilidumu kwa muda kisha baadaye hali ikakaa sawa na mgeni huyo akaendelea kuhutubia licha ya watu kumshangaa.
Ngwea aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini, Mei 28, mwaka jana, Jumatato iliyopita alitimiza mwaka mmoja tangu kifo chake.
Hadi sasa hati ya kifo chake haijatolewa hadharani licha ya familia ya msanii huyo kufanya juhudi za kuisaka kwa wahusika bila mafanikio.
0 comments:
Post a Comment