
STAA wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kifo cha msanii mwenzake Rachel Haule ‘Recho’ hakitafutika kichwani mwake kirahisi, kwa kuwa anamkumbuka kwa mengi.

“Amefanya kazi na RJ Company muda mrefu, baadaye akaamua kuanza kufanya kazi zake akishirikiana na Saguda. Mwanzo ulikuwa mzuri sana, alikuwa akitaka kitu chake anaweza kupiga simu hadi usiku kuomba ushauri. Kwa kweli sitamsahau, nitamlilia milele,” alisema Johari.
0 comments:
Post a Comment