Haikuweza kujulikana mara moja kisa ni nini haswa kilichofanya
Mtangazaji na Msanii wa muziki wa Bongo fleva,Jokate kuchukua deal
ambalo awali alikuwa ameshachukua Mtangazaji, Vanessa Mdee maarufu kama
Vee money,ni deal la kutangaza katika moja ya show mpya ya kipindi cha
kituo kipya cha TV1 iliyozinduliwa hii leo hapa Town,habari zinasema
kuwa awali baada ya Vanesa kuchukua deal hilo na alikuwa ameshaanza
kurekodi baadhi ya vipindi vya show hiyo mpya.

Show kama hiyo inayorushwa kwenye kituo cha televishen cha Viasat cha
huko nchini Ghana, ambacho zote pamoja na TV1 ipo chini ya kampuni moja
ya MTG ya nchini Sweden.Version ya kipindi hicho kitakuwa kinarushwa
hapa Tanzania kuanzia sasa, kitakachokuwa kinasimamiwa na mtangazaji
Jokate Mwegelo, pamoja na mtangazaji wa zamani wa Kiss Fm na Times
FM,Eden Jumanne maarufu kama The Rocker.
0 comments:
Post a Comment