UTAJIRI: Fedha za usajili wa Domayo zinaweza kukupa mali hizi
KWA mashabiki wa Yanga haikuwa taarifa nzuri. Iliwashitua mno
pale waliposikia kuwa kiungo wao mashuhuri, Frank Domayo, amejiunga na
mabingwa wapya wa Ligi Kuu Bara, Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Domayo alisaini Azam akiwa mchezaji huru baada ya
mkataba wake na wana Jangwani hao kubakiza mwezi mmoja tu hivyo kikanuni
alikuwa huru kuzungumza na hata kukubaliana na timu nyingine. Kanuni
zinatoa uhuru huo kwa mchezaji ambaye amebakiza chini ya miezi sita
katika mkataba.
Kiungo huyo anayeichezea pia timu ya taifa, Taifa
Stars, ameng’olewa Yanga kwa kitita cha Sh70 milioni huku na pia atakuwa
akilipwa mshahara wa Sh3 milioni kwa mwezi achilia mbali posho na juisi
za Bakhresa pale Chamazi.
Kwa maisha ya sasa ya Kitanzania, Sh70 milioni
alizolipwa ni fedha nyingi na ni wananchi wachache wa nchi hii
wanaofanikiwa hata kuzitia tu machoni fedha hizo kabla ya kurudisha roho
zao kwa Muumba achilia mbali kuzimiliki.
Hivi ni baadhi tu ya vitu ambavyo unaweza kuvifanya kwa fedha za usajili wa Domayo.
1.Kununua kiwanja
Kiasi cha Sh10 milioni kutoka kwenye kitita hicho
kinaweza kukupatia kiwanja cha maana cha ukubwa kati ya mita 25 kwa 25
au hata cha mita 35 kwa 35 katika maeneo tulivu ya Jiji la Dar es Salaam
kama vile Tabata, Tegeta, Kimara, Goba au Mbagala.
2.Shamba la ekari 2 Mlandizi, Pwani
Ardhi ni amana kubwa kwenye ulimwengu wa sasa, ni
amana ya kudumu. Hivyo ni vyema kwa mtu yeyote kuwekeza kwenye sekta hii
kwa ajili ya matumizi yake na ya uzao wake wa baadaye.
Katika fedha za Domayo kwenda Azam, unaweza
kutenga kiasi cha Sh 5 milioni pekee kununua kati ya ekari moja hadi
mbili za shamba katika maeneo ya Mlandizi au Kigamboni.
3.Toyota Hiace
Wafanyabiashara watakwambia kuwa fedha iliyokaa si
sawa na fedha iliyoko kwenye mzunguko. Kwenye fedha za usajili wa
Domayo unaweza pia kuchukua milioni 16 na kununua gari aina ya Toyota
Hiace kwa ajili ya biashara. Gari hizi zina uwezo wa kuingiza kati ya
Sh40,000 hadi 60,000 kwa siku hivyo kuwa kati ya uwekezaji wa maana
zaidi kwenye ulimwengu wa sasa unaohitaji zaidi usafiri.
0 comments:
Post a Comment