Rooney ajaa wasiwasi Manchester United
STRAIKA, Wayne Rooney amebainisha wasiwasi wake juu ya mpango wa
Manchester United wa kutaka kumpa kazi ya ukocha Louis van Gaal kwa
sababu jambo hilo litamweka kwenye wakati mgumu na Robin van Persie
atapata upendeleo.
Staa huyo wa Man United anaamini Van Gaal na Van
Persie ni marafiki wakubwa, hivyo akitua klabuni hapo anaweza kubadili
mambo ya kumpanga staa huyo kama chaguo la kwanza kwenye safu ya
washambuliaji na hali itarudi kama ilivyokuwa kwa Sir Alex Ferguson
msimu uliopita.
Rooney chini ya Ferguson alikuwa chaguo la pili
kwenye safu ya ushambuliaji nyuma ya Van Persie jambo lililomfanya staa
huyo kutaka kuhama kabla ya David Moyes kuja kumaliza tatizo.
Kwa hali ilivyo kwa sasa, Van Gaal anapewa nafasi
kuwa ya kuwa kocha mpya wa timu hiyo jambo ambalo limempa furaha kubwa
Van Persie ambaye kwa sasa amerudi mazoezini akitokea kwenye majeruhi
katika kipindi cha Moyes.
Van Gaal anaonekana kuwa ndiye kocha mwenye nguvu
zaidi ya kutua klabuni hapo baada ya kocha mwingine, Carlo Ancelotti
kuwa na uhakika wa kubaki Real Madrid kufuatia kuisaidia kutinga fainali
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment