Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akitoa hotuba juzi jijini Arusha.
Arusha. Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeelezwa kuwa
mfano halisi unaothibitisha uwezekano wa kuanzishwa na kudumu kwa
Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).
Wakuu wa nchi za EAC waliokutana jijini hapa jana
waliipongeza Tanzania kwa kuadhimisha miaka 50 ya Muungano huo Aprili
26, mwaka huu na kusema huo ni mfano wa kuigwa kwa ajili ya kusonga
mbele katika mikakati yao ya kuunda shirikisho la EAC. Akizungumza
wakati wa mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alisema kama
Tanganyika na Zanzibar zimeweza kuungana kwa miaka 50, hakuna sababu ya
Shirikisho la EAC kushindikana.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, Rais Yoweri Mseveni wa Uganda, makamu wa kwanza wa rais wa
Burundi, Prosper Bozombaza na waziri mkuu wa Rwanda, Dk Pierre
Habumuremy.
“Nachukua fursa hii kwa niaba ya viongozi wenzangu
kuwapongeza Rais Kikwete na Watanzania wote kwa kudumisha Muungano wao
ambao ni wa kipekee kwa bara la Afrika,” alisema Rais Kenyetta.
Kiongozi huyo aliwataka Watanzania kuulinda na
kuudumisha Muungano huo ambao ni darasa la namna ya kuungana wakati huu
wa mchakato wa kuanzisha shirikisho la kisiasa la nchi za Afrika
Mashariki.
Kwa sasa Tanzania iko kwenye mchakato wa kuandika
Katiba mpya na suala la muundo wa Muungano ndio linaonekana kutawala
mjadala huo kutokana na baadhi ya watu kutaka muundo ubadilike na kuwa
wa serikali tatu, huku kundi linaloongoizwa na chama tawala, CCM
likitaka kudumisha muundo wa serikali mbili ulioboreshwa.
0 comments:
Post a Comment