Funga kazi: Hao Man United usipime; Cavani, Strootman na Hummels wakitua ni balaa.
KOCHA Mdachi, Louis van Gaal, anapewa nafasi kubwa ya kutua Old
Trafford. Familia inayoimiliki klabu ya Manchester United ya Glazer
imeweka mezani Pauni 150 milioni kwa ajili ya kufanya usajili tu.
Jambo hilo tayari limeanza kuwatia kiwewe
mashabiki wa Man United juu ya mwonekano wa kikosi chao kwa msimu ujao
na kuwa na hamu mambo yatakavyokuwa baada ya msimu huu kila kitu kwenda
kombo.
Kocha Van Gaal anatarajiwa kutimua mastaa kadhaa
klabuni hapo na kuwaleta wengine wapya wachache ambao watakuwa tayari
kurudisha makali ya timu hiyo kama zamani.
Hiki ni kikosi cha kufikirika cha Man United
itakavyokuwa wakati wa msimu mpya utakaoanza Agosti mwaka huu. Kwa
kuanza na wachezaji wapya wanaotarajiwa klabuni hapo na wale wa zamani
watakaobaki kikosini.
Edinson Cavani
Straika huyo wa Uruguay kwa sasa anakipiga katika
kikosi cha Paris Saint-Germain ya Ufaransa. Thamani yake inatajwa kuwa
ni kati ya Pauni 55 milioni hadi 60 milioni.
Cavani hana furaha sana klabuni PSG, hasa kutokana
na Zlatan Ibrahimovic ambaye anamfanya apangwe pembeni badala ya nafasi
yake anayoipenda ya straika wa kati. Kwa siku za karibuni, Cavani
amekuwa kwenye ubora mdogo na hilo lilijionyesha zaidi katika mechi ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea iliyofanyika Stamford Bridge.
Imeelezwa kwamba watu wa Man United wameshafanya
mazungumzo ya awali na wawakilishi wa straika huyo kuhakikisha anang’oka
PSG, ambapo klabu hiyo italazimika kuvunja benki yake kwa sababu
hatapatikana kwa gharama ndogo.
Cavani alikuwa mchezaji wa sita ghali duniani
wakati alipotoka Napoli kwenda PSG kwa uhamisho wa Pauni 52.7 milioni
mwaka jana na kama atatua Old Trafford mahali hapo atapata fursa ya
kucheza kama straika wa kati kitu anachokikosa PSG.
Luke Shaw
Thamani ya beki huyo kinda wa Southampton inatajwa
kuwa Pauni 30 milioni. Kwa muda mrefu Man United imekuwa ikimtaka
mchezaji huyo ili kuwa mrithi wa Patrice Evra kwenye beki ya kushoto na
wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa kuipata huduma yake.
Kwa msimu wote, Shaw amekuwa chaguo la kwanza
katika kikosi cha Southampton jambo lililozifanya klabu kubwa za Ulaya
ikiwamo Chelsea, Manchester City, Bayern Munich na Real Madrid kufukuzia
saini yake. Inaaminika kwamba Shaw atakuwa na uhakika wa namba kama
atakubali kutua Old Trafford
0 comments:
Post a Comment