Sunday, May 11, 2014

MWILI WA MTU WAOKOTWA MTO MZINGA, KONGOWE JIJINI DAR

Mwili wa mtu huyo ukielea kwenye maji ya mto Mzinga.

Mwili baada ya kutolewa nje kabla ya kuzikwa na jiji.
Kamera yetu leo hii imenasa mwili wa mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake ukielea ndani ya Mto Mzinga maeneo ya Kongowe jijini Dar es Salaam.
Mwili wa mtu huyo ulipatikana baada ya wakazi wa eneo hilo kudai kuwa harufu kali ilikuwa ikitoka eneo hilo na ndipo waligundua maiti hiyo ambayo waliikuta ikiwa imeharibika kwa kiasi kikubwa.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe