Sunday, May 11, 2014

SHULE YA MWALIMU NYERERE YAVAMIWA NA KUNGUNI

Baadhi ya majengo ya Shule ya Sekondari ya Pugu yakiwa katika hali ya uchakavu.
    Waandishi wa GPL wakiwa shuleni hapo wakiongozwa na mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo.
Kibao cha Shule ya Sekondari ya Pugu.
SHULE ya Sekondari ya Pugu, iliyopo maeneo ya Pugu jijini Dar es Salaam, ambayo inasifa kubwa nchini kwa kuwa iliwahi kufundishwa na Baba wa Taifa, hayati Julius Kambarage Nyerere,  imevamiwa na wadudu aina ya kunguni ambao wanadaiwa kuwasumbua wanafunzi wa bweni wa shule hiyo.
Akizungumza na waandishi wetu, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Agustino Angelo, alisema tatizo hilo limekuwepo muda mrefu na wamejitahidi kulipunguza kwa kiasi kikubwa kwa kufanya upuliziaji (fummigation) mara mbili huku naye Mstahiki Meya wa Ilala Jerry Slaa, akiahidi kulimaliza kabisa tatizo hilo katika siku za hivi karibuni.
Waandishi wetu walizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, ambao walikiri kusumbuliwa na tatizo hilo ambalo wanadai kuwa linawakosesha amani na kuwataka viongozi wa serikali wajitokeze kutokomeza tatizo hilo ili waendelee na masomo yao vizuri.
Mbali na hayo, waandishi wetu pia walishuhudia majengo chakavu ya shule hiyo, mazingira ambayo si rafiki na heshima ya shule hiyo yenye historia kubwa nchini.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe