Pep Guardiola ajibebesha lawama kichapo cha Bayern
Pep Guardiola
PEP Guardiola amekubali yaishe na kujibebesha lawama zote baada
ya Bayern Munich kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa aibu kubwa
kufuatia kuchapwa na Real Madrid mabao 4-0 uwanjani kwao Allianz Arena
juzi Jumanne usiku.
Kwa kipigo hicho kilichowafanya miamba hiyo ya
Ujerumani kuutema ubingwa wa Ulaya, timu hiyo imekomea nusu fainali
wakiwa wamechapwa mabao 5-0, kitu kinachotazamwa na Wahispaniola kama
kisasi baada ya msimu uliopita timu hiyo kuitupa nje Barcelona kwa jumla
ya mabao 7-0 katika hatua kama hiyo.
Kwenye mchezo huo, Guardiola na kikosi chake
walipata somo kubwa juu ya soka la kushambulia kwa kushtukiza ambalo
lilichezwa na Real Madrid chini ya kocha wake, Mtaliano Carlo Ancelotti.
Mastaa Sergio Aguero na Cristiano Ronaldo kila
mmoja alifunga mara mbili kuwadhalilisha mabingwa hao wa Ulaya mbele ya
mashabiki wao uwanjani Allianz Arena na kocha Guardiola alisema
waliadhibiwa kwa sababu walishindwa kuufanyia haki mpira wakati
ulipokuwa kwenye miguu yao.
“Sababu kubwa ya kufungwa kwetu ni kwa sababu
hatukuwa na mpira sana. Kule Manchester na hata Madrid tulikuwa vizuri
sana uwanjani, lakini si kwenye mechi hii,” alisema Guardiola.
“Kama unashindwa kumiliki mpira, basi huwezi kuwa na nafasi unapocheza na timu kama hii (Real Madrid).
“Tulicheza vibaya na hilo ni wajibu wangu.
Tulikuwa juu sana na kichapo hiki ni ajabu. Nitakachofanya sasa
mazoezini ni kurudisha morali ya wachezaji ndani ya timu.”
0 comments:
Post a Comment