Msuva: Nina siri tatu hamzijui
Msuva alikuwa akilaumiwa kwa makosa kadhaa
mzunguko wa kwanza msimu uliopita lakini baadaye akabadilika na
akamaliza ligi akiwa tegemeo kikosini.
Alipozungumza na Mwanaspoti, Msuva alisema:
“Kwanza nilijifunza kitu kuwa mashabiki wanataka mambo mazuri tu na siyo
mabaya. Kupitia wao nikawa kila ninapokuwa uwanjani, nahakikisha
najituma kwa nguvu zangu zote na kurekebisha makosa yote ambayo nilikuwa
nayafanya nao wanayakemea ili nisiwaangushe.”
“Pili nimekuwa nafanya sana mazoezi yangu binafsi
mbali na yale ninayokuwa nafanya pamoja na timu, hata kama ninapokuwa
kambini huwa nafanya na zaidi ni kukimbia kutengeneza stamina na kasi
ndiyo maana uwanjani nakuwa fiti,”alisema Msuva.
“Lakini cha tatu ni kufuata maelekezo ya kocha kwa
kutimiza kila kitu ambacho anakihitaji. Kama unavyojua kila kocha
anastahili yake ya ufundishaji, vile unavyomfuata ndiyo unakwenda naye
sawa,”alisema Msuva ambaye uwepo wake umeongeza kasi kwenye fowadi ya
Yanga hasa anaposimama na winga mwenzake, Mrisho Ngassa.
0 comments:
Post a Comment