Aliyemrushia ndizi Alves adakwa na polisi
SHABIKI wa Villarreal anayedaiwa kumrushia ndizi beki wa
Barcelona, Dani Alves uwanjani Jumapili iliyopita, amekamatwa na polisi
nchini Hispania.
Shabiki huyo aliwekwa chini ya ulinzi na kubanwa
kwa maswali mazito huku klabu ya Villarreal ikimfungia maisha yake yote
kwenda kutazama mechi za klabu hiyo.
Kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Barcelona
kushinda 3-2 uwanjani Estadio El Madrigal, shabiki huyo alirusha ndizi
uwanjani katika dakika ya 75 akimlenga Alves aliyekwenda kupiga kona.
Katika kujibu ubaguzi huo, Alves aliiokota ndizi hiyo akaimenya na
akaila kabla ya kupiga kona.
Msemaji wa polisi alisema mtu huyo alikamwa na polisi na kuwekwa rumande tangu wikiendi iliyopita.
0 comments:
Post a Comment