Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akikagua nyumba hiyo ya zamani iliyokuwa inatumiwa na
Mfugaji Mihangwa, kabla ya kujenga nyumba ya kisasa katika Kijiji cha
Heka, wilayani Manyoni Singida.
Kinana akiangalia
mifungo ya Mfugaji Mihangwa iliyobakia baada ya kuuza mingine kwa ajili
ya kujenga nyumba ya kisasa. Mihangwa anasema aliamua kuuza ng'ombe 200
kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ya kisasa.
Kinana akizindua nyumba Mfugaji huyo ya kisasa kabisa . Kulia ni Mfugaji Mihangwa mmiliki wa nyumba hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana (haonekani pichani) na wajumbe wengine wakitoka nje ya nyumba ya
kisasa ya Mfugaji Mihangwa mara baada ya kuikagua,Bwan.;Mihangwa aliuza
ng'ombe zake 200 na kubaki na ng'ombe 100 kwa ajili ya ujenzi wa
nyumba hiyo ya kisasa kama ionekanavyo pichani.
jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka kama lionekanavyo pichani
Kinana akisaidia
kumpatia tofali fundi wa jengo la maabara ya Shule ya Sekondari Heka
wakati wa ziara yake katika Jimbo ya Manyoni Mashariki. Kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligat
Kinana akilakiwa na mabango katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka wakati wa ziara yake wilayani Manyoni.
Nape akihutubia katika
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Heka, ambapo aliwaambia wananchi
kuwapuuza wapinzani kwani hata wakifanya mkutano hawasaidii wananchi
katika masuala ya maendelo, bali wamebaki wakihubiri suala ya Katiba
Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana akimtambulisha Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki,Kapt.John
Chiligati kwa wananchi wa Kijiji cha Heka katika mkutano wa
hadhara.Aidha Mh.Chiligati alielezea katika mkutano huo miradi
mbalimbali iliyotekelezwa katika eneo hilo la Heka.
Wanachama wapya wakila
kiapo ha utii cha CCM baada ya kujiunga na chama hicho katika mkutano wa
hadhara katika Kijiji cha Heka, Manyoni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana akishiriki mazoezi ya Wanafanzi walioko kambini kwa ajili ya
mashindano ya UMISSETA wilaya ya Manyoni jioni ya leo mkoani Singida.
Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia kwenye mkutano wa hadhara ambao
pia ulihudhuriwa na Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Stendi ya
Manyoni, willayani Manyoni, Singida leo. Nape amesema kitendo cha vyama
vya upinzani kuunda Ukawa umekirahisishia CCM kuvishambulia vyama hivyo
kwa pamoja badala ya kimoja kimoja.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatulia yaliyokuwa yakizungumzwa uwanjani hapo.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika Stendi ya
Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe
ya mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho,
tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi
kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa" alisema Kinana akatika mkutano
huo..
Mbunge wa Jimbo la
Manyoni Mashariki, Kapteni John Chiligati akiwahutubi wananchi wa mji wa
Manyoni mapema leo kwenye stendi ya mabasi Manyoni.
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Stendi ya
Manyoni, wllayani Manyoni, Singida leo. "Katiba tunaitaka, lakini isiwe
ya mazingaombwe ya kukoroga vichwa vya watu. ndugu msitoane macho,
tusing'oane meno kwa ajili ya katiba ambayo hata ikija mpya haiwezi
kugeuza chai ya rangi kuwa ya maziwa" alisema Kinana akatika mkutano
huo.Ndugu Kinana yupo mkoani humo kwa ziara ya siku 8 akitokea mkoani
Tabora ambako alikuwa na ziara ya siku 11.
0 comments:
Post a Comment