Azam Bus
AZAM Tv imefanya kufuru kwa kutoa udhamini wa Sh 361.6 milioni
kwa ajili ya kurusha ‘live’ mashindano ya mpira wa kikapu ya Miji Mikuu
ya Afrika Mashariki na Kati, ambayo yanaanza leo Jumanne Uwanja wa Ndani
wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yatafanyika kwa siku sita kuanzia
leo Jumanne mpaka Jumapili, Azam itakuwa inarusha mechi zote kuanzia saa
2 asubuhi mpaka saa 2 usiku mechi hizo zinapomalizika kwa mujibu wa
ratiba ya mashindano hayo.
Kurusha mechi moja kwa saa moja ni Dola 3,000 (Sh
4.8 milioni) ambapo kwa saa 12 itakuwa ni Sh57.6 milioni na hivyo kwa
siku sita ni sawa na Sh345.6 milioni. Imeelezwa kuwa Azam wameahidi
kusaidia bajeti ya Sh16 milioni ambayo waandaji walipeleka hivyo kufika
kiwango cha Sh 361.6 milioni.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Mwenze
Kabinda, alisema; “Bajeti yetu ilikuwa ni Sh16 milioni ndiyo
tuliyopeleka kuomba kusaidiwa, lakini Azam wamechukua jukumu la
kutudhamini kurusha mechi zetu zote na kusaidia fedha tulizoomba. Sisi
tusingeweza kufanya hivyo kwani kiasi tulichoomba kilikuwa ni kwa ajili
ya maandalizi mpaka tutakapomaliza.”
Katika ufunguzi wa mashindano hayo timu ya jiji la
Dar es Salaam ambao ni wenyeji itaanza kampeni yake ya kusaka ubingwa
huo kwa kucheza na Mombasa katika mechi ya ufunguzi, Mbeya na Kigali,
Tanga na Adiss Ababa wakati upande wa wanawake, Dar es Salaam watacheza
na Kampala mechi hizo zitachezwa kabla ya ufunguzi rasmi wa michuano
hiyo.
0 comments:
Post a Comment