Mr Rage
KWA mujibu wa Katiba mpya ya Simba, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage, sasa ni Rais wa klabu hiyo.
Katiba ya Simba iliyokuwa kwa Msajili wa Klabu na
Vyama vya Michezo nchini imepitishwa rasmi huku cheo cha Mwenyekiti
ambacho Rage anacho kimebadilishwa na kuwa Rais. Rage ndiye Mwenyekiti
kwa sasa.
Kupitishwa kwa Katiba hiyo pia kunamaanisha kuwa
zoezi la uchaguzi wa klabu ya Simba limefunguliwa rasmi na leo Jumanne
Kamati ya Uchaguzi ya timu hiyo itakutana ili kujadili tarehe rasmi ya
kufanyika kwa uchaguzi huo pamoja na utaratibu utakaotumika.
Akitangaza kupokea katiba hiyo mpya Toleo la mwaka
2014, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kipengele cha 26
kilipendekezwa na wanachama wa klabu hiyo kumruhusu mtu aliyewahi
kushtakiwa kwa makosa ya jinai kugombea, kiliondolewa na kurejeshwa kile
cha awali kilichokua kikitaza suala hilo kama ilivyoelekezwa na TFF.
Katibu huyo aliongeza kuwa katiba hiyo mpya pia
imeongeza kipengele cha Kamati ya Maadili na Rufaa ambayo itatangazwa
wiki hii na itakua ikishughulikia masuala ya maadili pamoja na kutoa
fursa ya wanachama wa timu hiyo kukatia rufaa maamuzi mbalimbali ambayo
hawajaridhishwa nayo.
0 comments:
Post a Comment