Domayo awaponza wachezaji Stars
UKIFIKA katika kambi ya Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ mjini Tukuyu
unatakiwa ujipange, kwani ulinzi umeimarishwa na wachezaji hawazungumzi
ovyo na mtu wasiyemfahamu wakiogopa kuadhibiwa na TFF.
Hali hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Frank
Domayo kusaini mkataba wa kuichezea Azam akiwa katika kambi hiyo baada
ya watu kuingia kinyemela na kumalizana naye.
TFF haikupendezwa na kitendo hicho kiasi cha Rais wake, Jamal Malinzi kuteua mwanasheria wa kuchunguza sakata zima la Domayo.
Mwandishi wa Mwanaspoti, alifika kambini hapo na
kukumbana na maswali kadhaa tofauti na awali na hata alipoomba ruhusa ya
kuzungumza na baadhi ya wachezaji kutoka kwa Meneja wa Taifa Stars
inayojiandaa na mechi dhidi ya Zimbabwe, Clemence Boniface.
‘’Huyu ni mwandishi, anaomba kuzungumza nanyi
kuhusu maandalizi yenu, mpeni ushirikiano,’’ alisema Clemence lakini
baadhi ya wachezaji walijibu: ‘’Sawa meneja una hakika huyu si wale
wanaoweza kutuponza? Maana wengine wanatuponza.’’
Baadhi ya walinzi na wahudumu wa kambi hiyo,
walisema tangu sakata la Domayo wachezaji wamebadilika, hawataki
kuzungumza na watu wasiowajua wakihofu kutokea mambo kama hayo
0 comments:
Post a Comment