Van Persie abadili mawazo Man united
STRAIKA, Robin van Persie, amefichua kwamba sasa amefuta mpango
wake wa kutaka kuhama Manchester United baada ya klabu hiyo kumtimua
David Moyes huku Mdachi mwenzake, Louis van Gaal akitarajia kuwa kocha
mpya klabuni hapo.
Ripoti zinabainisha kwamba Van Gaal amekubali kuwa
kocha wa Man United baada ya kukutana na mabosi wa klabu hiyo zaidi ya
saa 48 zilizopita na kwamba anajiandaa kuwa mrithi wa Moyes klabuni hapo
Old Trafford.
Si kitu cha siri kwamba Van Persie amekuwa na
urafiki mkubwa na Van Gaal ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi
na hilo ndilo linalomfanya straika huyo kubadili mawazo yake na kusema
ataendelea kubaki Old Trafford msimu ujao.
Van Persie aliweka wazi wiki chache zilizopita
kwamba kama Moyes angeendelea kuwa kocha wa timu hiyo, basi angelazimika
kutafuta timu ya kuchezea mwisho wa msimu na si kubaki Man United chini
ya kocha huyo Mskochi.
Van Persie na Van Gaal wanasimamiwa na wakala
mmoja, Kees Vos, ambaye siku chache zilizopita alikuwa kwenye
pilikapilika nyingi za mazungumzo na mabosi wa Man United
0 comments:
Post a Comment