Joseph Warioba: Nishani yangu haihusiani na Katiba
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Nishani ya Kuuenzi
Muungano aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete, haina uhusiano wowote na
yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema hayo alitakiwa kueleza furaha
yake baada ya Rais Kikwete kutambua mchango wake kwa Taifa na kuamua
kumtunuku nishani hiyo Jumamosi iliyopita Ikulu.
“Sikupewa nishani ile kwa sababu ya mchakato wa
Katiba. Nishani ile inahusu miaka 50 ya Muungano, msihihusishe na
mchakato wa Katiba,” alisema.
Jaji Warioba ambaye amewahi kulieleza gazeti hili
kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipendekeza muundo wa serikali tatu
kwa ajili ya kuunusuru Muungano, alisema baadhi ya wananchi
wamelitafsiri suala hilo kisiasa.
Alisema kuwa tume yake ilipendekeza muundo wa
serikali tatu kutokana na maoni yaliyotolewa na wananchi na kusisitiza
kuwa jambo hilo haliwezi kuhusishwa na nishani aliyopewa.
“Rasimu ya Katiba imekusanya maoni ya wananchi na
ndiyo maana tume ikapendekeza muundo ule. Sasa suala hili lisihusishwe
na nishani kwani ni vitu viwili tofauti,” alisisitiza.
Wakati akipewa nishani hiyo, Jaji Warioba
alisifiwa kuwa ni mmoja wa viongozi waliouenzi Muungano kupitia nyadhifa
mbalimbali alizoshika wakati akiwa mtendaji mwandamizi wa Serikali.
Tangu Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikabidhi Rasimu
yake Desemba 30 mwaka jana, imekuwa ikipingwa kila kona na makundi
mbalimbali hasa la wanaCCM ambao wanapigia debe muundo wa serikali
mbili.
Baadhi ya viongozi wa chama hicho wamekuwa
wakitamka wazi kuwa muundo wa serikali tatu unaopendekezwa na Tume ya
Jaji Warioba ni tishio kwa uhai wa Muungano.
Mtizamo kuhusu muundo huo pia ulizua msuguano
katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana baadhi ya wajumbe wake kutoa
lugha za kejeli na kuudhi kwa Jaji Warioba, wakidai kuwa ni msaliti
0 comments:
Post a Comment