Muungano ulivyowavuruga Wazanzibari
Hija Hassan Hija akichangia
Wiki hii Watanzania wameshuhudia matukio mengi bungeni. Moja ya
matukio hayo ni vita ya maneno na tofauti za kisiasa kati ya CUF na CCM.
Vita hiyo kuhusu aina ya mfumo wa Muungano
imewagawa vilivyo Wazanzibari. Kwa siku mbili mfululizo wamevutana juu
ya kilichopendekezwa kwao kati ya serikali tatu, mbili au muungano wa
mkataba.
Mmoja wa wajumbe hao akawatuhumu Mawaziri wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kukana misimamo yao ya awali ya
kutaka serikali tatu.
Mjumbe aliyeonekana mwiba kwa mawaziri hao ni Hija Hassan Hija.
Pamoja na mambo mengine akasema kabla hawajapewa
uwaziri walikuwa wakidai serikali tatu, sasa wanaufyata na kusimama
kwenye serikali mbili.
Hija ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kiwani (CUF),
aliwatuhumu baadhi ya Mawaziri wa SMZ kuwa ni “wasaka tonge” na wanafiki
akisema mawaziri wa aina hiyo ni hatari kwenye jamii.
“Kuna watu wanalinda masilahi yao… iwapo leo
Mawaziri wa Zanzibar (akiwaonyesha kwa vidole ndani ya Bunge)
utawanyang’anya uwaziri, watadai serikali tatu,” anasema na kuongeza.
“Wenzangu ni mashahidi… Mawaziri wote wa Zanzibar
wamekuwa wakisema hadharani kuwa muundo huu wa Muungano unatuonea, leo
wamepatwa na nini?” anajibu kwa kusema ni kwa sababu ya masilahi
binafsi.
Anabainisha kwamba mawaziri hao ndiyo waliofanya
mabadiliko ya 10 ya Katiba visiwani humo, baada ya kauli ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda iliyosema Zanzibar siyo nchi.
Mjumbe huyo anasema amemweleza Waziri, Profesa
Mark Mwandosya kuwa mawaziri hao wa Zanzibar hawatetei muungano bali
masilahi yao.
“Zanzibar hatuna ubaguzi wa kabila wala dini tuna
mgogoro wa wasaka tonge ambao hawajashiba, mkiwafuata hawa muungano huu
utakufa, wana mitumbo mikubwa lakini wana njaa,”anaeleza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Utawala
Bora Zanzibar, Mwinyi Haji Makame baada ya kuruhusiwa kuchangia mjadala
bungeni akaituhumu CUF kuwa inataka serikali ya mkataba ili ivunje
muungano
0 comments:
Post a Comment