Chipukizi Mtanzania kwenda Barcelona
Nick Van Lawick (13 , ambaye ni chotara anayetokana na mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji mkubwa kama anavyoota,
Siku zote katika maisha ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuheshimu
ndoto zetu hata kama tunadhani ni ndoto ndogo. Kuziheshimu ndoto zetu
na kuzitimiza, kunahitaji nidhamu ya ziada, ingawa wapo wanaozifikia
andoto zao kwa bahati.
Wengi husema wanataka kutimiza ndoto zao, lakini
ni wachache hufanikiwa kutimiza ndoto zao. Hata hivyo kwa kuwa binadamu
tuna ndoto tofauti tofauti ni ngumu kuwa na kanuni moja ya jinsi ya
kufikia ndoto zetu.
Mtoto Nick Van Lawick (13), anayesoma shule ya
kimataifa ya Dar es Salaam Independence School, ana ndoto ya kuichezea
klabu ya Barcelona ya Hispania na anatarajia atatimiza ndoto hiyo.
Hiyo inatokana na kipaji alichonacho cha soka na
mipango iliyofanywa na wazazi wake, ambao watamkutanisha Nick na
mtaalamu wa viungo wa klabu ya Barcelona, Juanjo Brau.
Baba mzazi wa Nick anayeitwa Hugo van Lawick anasema: “Nick amepata nafasi ya kwenda kupewa mafunzo na Brau.
“Mama yangu Jane Goodall ni rafiki wa karibu wa
Brau na mama yangu anafahamu kipaji cha mpira cha mjukuu wake, ndio
maana aliona awasiliane na rafiki yake kuangalia nafasi ambayo Nick
anaweza kujiendeleza zaidi kisoka.
“Brau alishauri kuwa Nick aanze kwa kumpa mafunzo
ndipo mchakato wa kumtafutia nafasi katika timu ya vijana ya Barcelona
ufanyike.”
Kwa upande wake Nick, anayesoma kidato cha pili,
anasema anapenda sana mpira na muda wake mwingi huutumia katika mambo
yahusuyo mpira huku akiipenda zaidi klabu ya Barcelona kwa sababu ya
staili yao ya uchezaji.
Aota kuisaidia Tanzania
Nick (pichani), ambaye ni chotara anayetokana na
mzazi wa Kijerumani na Kitanzania, anasema akikua na kuwa mchezaji
mkubwa kama anavyoota, atatumia sehemu ya fedha atakazopata kusaidia
mambo mbalimbali nchini, hasa hasa tatizo la umeme na kusaidia watoto
walio kwenye mazingira magumu.
RSS Feed
Twitter
10:57 PM
Unknown
0 comments:
Post a Comment