Monday, April 28, 2014

Barkley atishiwa maisha, kisa demu

0
Share

KIUNGO wa Everton, Ross Barkley, ametishiwa maisha na jambazi na muuza dawa za kulevya, Sam Walker kutokana na ugomvi unaotakana na mwanamke.
Walker, 30, alimtumia ujumbe kwenye Twitter kiungo Barkley akimpiga marufuku kabisa kujisogeza kwa mrembo ambaye hakumtaja na kusema maisha yake ya soka yatakatika ghafla.
Ripoti zinabainisha kwamba mpenzi wa zamani wa Barkley kwa sasa ana uhusiano wa kimapenzi na Walker na wasiwasi wa jambazi huyo ni kitendo cha kiungo huyo kutumiana meseji na mrembo huyo.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mirror, Barkley na Walker hivi karibuni walikutana kwenye ukumbi mmoja wa starehe za usiku huko Liverpool na kujadiliana. Ukumbi huo upo katika eneo ambalo mke wa Peter Crouch mrembo, Abbey Clancey na wa Steven Gerrard, Alex, wanapenda sana kwenda.
Maofisa polisi kutoka Merseyside walithibisha kuzungumza na Barkley baada ya kupokea simu kutoka kwa mtu mwingine aliyetoa malalamiko kwamba mchezaji huyo ametishiwa maisha.

 

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe