Kumbe Van Gaal ni mwendawazimu namna hii!
WAKATI Manchester United itakapomtangaza, Lous Van Gaal kuwa
kocha wao mpya pale Old Trafford, usije ukadhani kwamba watakuwa
wamemchagua kocha mstaarabu na mpole. Hapana, watakuwa wamemchagua kocha
mwendawazimu aliyepitiliza.
Awavulia bukta wachezaji wake
Kama maigizo hivi. Lakini katika tukio moja
lililotokea wakati wa msimu wa 2009/10 akiwa na Bayern Munich ya
Ujerumani, Van Gaal alifanya kituko cha ajabu kwa kuvua suruali yake
mbele ya wachezaji wa Bayern kuwaonyesha kuwa yeye alikuwa mwanamume
shababi na mwenye makende. Mshambuliaji wa zamani wa Italia, Luca Toni,
anaelezea tukio hilo.
“Kocha alitaka kutuonyesha wazi kwamba anaweza
kumwacha nje mchezaji yeyote yule. Alitaka kuashiria kwamba alikuwa na
kende. Alifanya hivyo kwa kuvua suruali yake. Sikuwahi kuona kitu kama
hicho maishani, ulikuwa ni ukichaa. Sikuona vizuri sehemu zake za siri
kwa sababu sikuwa mbele,” anasema Toni.
Kwa mtindo huu, Wayne Rooney na Robin Van Persie wajiandae!
Amfukuza Rivaldo Barcelona
Wakati Van Gaal aliporudi Barcelona mwaka 2002,
moja kati ya kazi zake za kwanza ilikuwa kumfukuza Rivaldo, mchezaji
ambaye hakuwa na uhusiano naye mzuri kabisa. Hii ilikuwa ni moja kati ya
majibu yake kwa Rivaldo ambaye aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari
akisema: “Simpendi Van Gaal na Van Gaal hanipendi.”
Baadaye Van Gaal aliripotiwa akidai kuwa madai ya Rivaldo hayakuwa ya kweli.
“Nampenda Rivaldo hasa yule wa kabla ya kutwaa
uanasoka bora wa Dunia mwaka 1999. Nilimpenda Rivaldo. Nilimpenda sana
kwa sababu alikuwa bora. Lakini kuanzia hapo kwenda mbele hakuweza
kuhimili mapigo. Si katika soka tu, bali hata katika maisha yake
binafsi. Hata ukiangalia kwa makocha wengine, kiwango cha Barcelona
kimeporomoka,” alisema.
“Nilimpenda Ronaldo aliyejituma. Kwa sasa hajitumi
kabisa. Kiwango chake Barcelona kimeshuka tofauti na anapokuwa na
Brazil. Nilipomwona Rivaldo na Brazil alikuwa ana njaa, anajituma.”
Aidharau Barcelona
Van Gaal alipata mafanikio makubwa akiwa katika
soka la kwao Uholanzi ambako alitwaa Kombe la Uefa, taji la Ligi ya
Mabingwa Ulaya na mataji matatu ya Ligi Kuu Uholanzi ‘Eredivisie’.
0 comments:
Post a Comment