Boat ya Seagul yagonga jahazi.
Boat ya Seagul inayofanya safari zake kati ya
Zanzibar na Dar Es Salaam, imegonga jahazi mchana wa leo ambalo lilikuwa
likitokea Zanzibar kuja Dar Es Salaam.
Inasemekana kuwa jahazi hilo lilipunguza sana mwendo
kutokana na upepo kubadili muelekeo ghafla. Nikiwa mmoja wa mashuhuda
tulishangaa kuona Boat ile ikija kwa kasi huku abiria wa kwenye Jahazi
wakipunga kuonyesha ishara kuwa hali si salama lakini Boat ilizidi
kwenda na mwendo ule ule kana kwamba hakuna kitu mbele yake. na ndipo
kishindo kikatokea na Jahazi lile lilikokotwa umbali wa takribani mita
200.
Hakuna aliye fariki kwani abiria wote waliokuwa
kwenye jahazi walijitosa baharini kabla ya ajali kutokea isipokuwa
wawili ambao walikokotwa na Jahazi lao lakini walifanikiwa kutoka kabla
halijazama.
Tanga la Jahazi likiwa limenasa mbele ya Boat ya Seagul baada ya kugongwa na kuanza kuzama baharini.
Boat ya Seagul baada ya kuligonga Jahazi ambalo lilikuwa likitokea Zanzibar mchana wa leo.
Jahazi lianza kuzama baada ya kutokea mpasuko baada ya kugongwa na Boat ya Seagul iliyokuwa ikielekea Zanzibar.
Sehemu ya Tanga ikionekana kwa mbali huku chombo kikiendelea kuzama baharini eneo la Ferry.
Ngalawa zikijaribu kuokoa baadhi ya watu waliokuwa
kwenye Jahazi ambalo inasemekana lilikuwa limesheheni makreti ya bia na
bidhaa nyingine likitokea Zanzibar.
Wavuvi wakijaribu kuokoa baadhi ya mali kutoka
jahazini huku Boat ya Seagul ikiwa imeondoka kuendelea na safari baada
ya kuona Jahazi limezama.
Picha hizi haziko clear sana nilipiga kutumia simu yangu ya mkononi.
0 comments:
Post a Comment