Bingwa wa kupanga sauti, miaka 53 jukwaani, nyimbo zaidi 200
Nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Maalim Gurumo
ULIMWENGU wa muziki umekumbwa na mshtuko, kufuatia kifo cha
nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Maalim Gurumo ambaye amefariki
dunia Jumapili iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na
kuzikwa kijijini kwake Masaki, mkoani Pwani juzi.
Gurumo amefariki kutokana na maradhi ya mapafu na moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Miaka 53 jukwaani
Nguli huyo ambaye ana heshima ya pekee katika
ulimwengu wa muziki nchini, amefariki baada ya utumishi wa miaka 53
mfululizo jukwaani akipumzika siku chache zikiwemo siku za Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani akiwa ametunga na kushiriki kuimba nyimbo nyingi sana.
Aidha, Gurumo ametunga mitindo mitatu ya muziki wa
dansi na miwili bado inatamba hadi sasa, mitindo hiyo ni Sikinde
unaotumiwa na Bendi ya Mlimani Park na Msondo Ngoma ambao ulikuwa
ukitumika na Bendi ya Nutta Jazz (ambayo ilibadilika kwa majina ya
Juwata Jazz, Ottu Jazz na sasa Msondo Ngoma).
Mtindo mwingine ni Ndekule ambao ulikufa baada ya
Bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS) kupotea katika muziki wa dansi na
kama si maradhi Gurumo angeshiriki jubilee ya miaka 50 akiwa na bendi
hiyo.
Bingwa wa kupanga sauti
Gurumo ameshiriki kutengeneza ‘arrange’ nyimbo
mbalimbali zilizotungwa na wanamuziki wengine kwa kuzisahihisha pale
alipohisi zina matatizo katika upigaji wa vyombo. Pia alipanga sauti za
waimbaji mbalimbali kutokana na maudhui ya wimbo husika na wengi
walimwamini katika hilo.
Mwanamuziki huyo alitangaza kustaafu mwishoni mwa
mwaka jana, ikiwa ni miezi mitatu kabla ya bendi yake ya Msondo Ngoma
haijatimiza miaka 50 ya kuwepo katika ulimwengu wa muziki nchini,
amefariki akiwa taswira na nembo ya muziki wa dansi nchini.
Tuzo ya heshima
Tofauti na wakongwe wenzake ambao wamekuwa
wakipumzika na kurudi tena jukwaani kama vile marehemu, Fatuma Binti
Baraka ‘Bi. Kidude’ kwa kufanya onyesho moja au mawili kwa mwaka, Gurumo
ana historia ya namna yake ambayo pengine haiwezi kufikiwa na yeyote
nchini na Afrika Mashariki.
Historia inamweka meza moja na wanamuziki wengine
nguri duniani kama vile, Mariam Makeba ambaye Rais wa Kwanza wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela alimtunuku tuzo ya Mama Afrika na Balozi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Yosssour Ndour
wa Senegal. Pia,
0 comments:
Post a Comment