Asilimia 20 ya bajeti hupotelea halmashauri
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Rajab Mbarouk Mohamed akizungumza Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa LAAC
Dar es Salaam. Wizi wa fedha za umma kwenye
halmashauri mbalimbali nchini unasababishwa na elimu ndogo ya baadhi ya
madiwani ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa fedha hizo, imeelezwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Serikali za Mitaa (Laac), Rajab Mbarouk Mohamed alisema jana kwamba
zaidi ya asilimia 20 ya fedha za bajeti hupotea kila mwaka kwenye
halmashauri. “Fedha hizi zinapotea kwa sababu madiwani ambao ndiyo
wasimamizi wakuu wameshindwa kudhibiti wizi wa fedha hizo,” alisema.
Mbarouk alisema wataalamu kwenye halmashauri hizo
wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kufanya ufisadi kwa sababu baadhi ya
madiwani hawana uelewa wa fedha wanazozisimamia.
Alisema halmashauri hizo zimekuwa zikipewa fedha
nyingi kuliko zinazotolewa kwa baadhi ya wizara. “Kwa hiyo tunapoteza
fedha nyingi kwa sababu madiwani wengi hawana elimu, tunahitaji
kubadilisha mfumo wa usimamizi wa fedha,” alisema Mbarouk.
Akitoa mfano alisema wakati kuna baadhi ya wizara
zinapata bajeti isiyozidi Sh3 bilioni kuna halmashauri ambazo zinapata
Sh15 bilioni.
“Hizi ni fedha nyingi ambazo zinahitaji usimamizi wa watu wenye elimu ya masuala ya fedha,” alisema.
Mbarouk alisema wakati umefika wa kuanza kutoa elimu kwa madiwani ili waweze kusimamia ipasavyo fedha za Serikali
0 comments:
Post a Comment