Monday, April 28, 2014

Moyes, mkewe wanaswa na mabegi yao Marekani

 

Moyes akiwa na mabegi akiwa na mkewe  

KOCHA, David Moyes, anataka kusahau majanga yake yaliyomkuta Manchester United baada ya kumchukua mkewe, Pamela na kwenda mapumzikoni Miami, Marekani.
Baada ya kocha huyo kufutwa kazi Man United Jumanne iliyopita na kisha Ryan Giggs kukabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hiyo hadi mwisho wa msimu na huku Man United ikiishinda Norwich City juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Old Trafford, Moyes alionekana Florida kwenye mgahawa mmoja akipata chakula cha jioni na mkewe.
Mwanzoni Moyes na Pamela walionekana na mabegi yao jijini Manchester wakiwa hawaeleweki wanakwenda wapi kabla ya picha za Jumamosi kuwaonyesha wakiwa Miami, Florida akijipumzisha kupoteza mawazo ya kufukuzwa kazi.
Akiwa kwenye meza ya chakula na mkewe, Moyes, mara kadhaa alionekana kubofyabofya simu yake huku wanoko wakidai kwamba alikuwa akitazama matokeo ya timu hiyo kwenye mechi yao dhidi ya Norwich City. Man United ilishinda 4-0

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe