Yaya Toure asema hawezi kwenda Real Madrid
Supastaa wa Ivory Coast, Yaya Toure anayekipiga katika timu ya Man City nchini England
HAPANA. Kamwe siwezi na sijawahi kuwaza. Nienda Real Madrid?
Haiwezekani. Amesisitiza supastaa wa Ivory Coast, Yaya Toure kwamba
kwenye maisha yake hajawahi kuwaza au kufikiria mpango wa kujiunga na
Real Madrid ya Hispania.
Kiungo huyo anayekipiga kwenye kikosi cha
Manchester City kwa sasa alisema hawezi kwenda Real Madrid kwa sababu
moyo wake na mapenzi yake yapo kwa Barcelona, klabu ambayo aliichezea
kabla ya kutua England. Yaya Toure alisema Catalunya ndiko moyo wake
ulipo na si Madrid.
“Mimi shabiki wa Barcelona, sitarajii kwenda Real Madrid,” alisema Yaya Toure alipozungumza na radio Rac-1 ya Catalan.
Wakati akijiandaa na mchezo wa marudiano wa hatua
ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Yaya Toure alisema
hatashangilia kama ataifunga Barcelona, kwa sababu ni timu anayoiheshimu
baada ya kudumu nao kwa miaka mitatu.
“Siwezi kuwakosea heshima. Watu wao siku zote
walikuwa wakinisapoti, hivyo siwezi kufanya kinyume. Ninachoshukuru ni
kwamba Barcelona wamenifundisha jinsi ya kushinda,” alisema.
0 comments:
Post a Comment