Simba yafanya usajili mpya kizungu
SI Azam FC tu inayofanya mambo kisayansi, hata Simba ya Msimbazi na yenyewe imeanza kubadilika.
Azam imeshamsainisha kiraka Owen Kasule wa Uganda
tayari kwa msimu ujao lakini Simba kupitia kwa mkurugenzi wake wa
ufundi, Moses Bassena inapitia viwanjani kukagua wachezaji wote kwenye
timu zote za Ligi Kuu Bara.
Kwa mujibu wa Simba hilo linafanyika ili
kuhakikisha wanafanya usajili wa maana na si magarasa kama ilivyokuwa
awali kwa kuwafuatilia kwenye mechi zao wanazocheza.
Basena raia wa Uganda aliliambia Mwanaspoti kuwa:
“Napenda kuja kuangalia mechi hizi kwa sababu namjua kila mchezaji hata
kama tukimhitaji tunajua uwezo wake uwanjani, kujua kiwango cha mchezaji
mwenye ubora ni baada ya kumwona kwenye mechi nne hadi tano na si
mchezo mmoja na ndiyo maana napenda kufuatilia kila mchezaji.”
Bosi huyo ambaye aliwahi kuwa kocha wa Simba,
amekuwa akibaki Dar es Salaam wakati timu yake ikiwa nje ya mkoa huo au
kusafiri mikoa ya jirani kuziangalia timu pinzani kwa lengo la kuzisoma
kiufundi na kumuongezea mbinu Logarusic na baadaye kuangalia wachezaji
muhimu ambao wanaweza kusajiliwa kwa ajili ya kikosi cha msimu ujao
0 comments:
Post a Comment