Man City vinara Kombe la Ligi
LONDON, ENGLAND
MPANGO wa kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini kutwaa mataji manne msimu huu umeanza kwa kubeba Kombe la Ligi baada ya kuinyuka Sunderland mabao 3-1.
Katika mechi hiyo ya fainali iliyochezwa jana
Jumapili kwenye Uwanja wa Wembley, Sunderland ndio waliokuwa wa kwanza
kupata bao dakika 10 mfungaji akiwa ni Rabio Borini.
Ushirikiano wa Yaya Toure na Pablo Zabaleta
uliipatia Man City bao la kwanza dakika 54, bao ambalo Yaya alilifunga
kwa shuti kali.
Dakika moja baadaye, Samir Nasri aliipatia Man City bao la pili akiujaza mpira wavuni baada ya kuinasa pasi ya Aleksandar Kolarov.
Dakika ya 89, Yaya alimuunganishia pasi safi Jesús Navas ambaye alifungia Man City bao la tatu.
Man City inakuwa imelibeba taji hilo mara ya tatu baada ya kufanya hivyo mwaka 1970 na mwaka 1976.
Kwa Pellegrini hilo ni taji lake la kwanza England
na hivyo anabakiwa na mtihani wa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
0 comments:
Post a Comment