Yanga na Simba zaingiza Sh139 milioni

Mabeki wa Rhino Ranges Salum Kamana (kushoto) na Ladislaus Mbogo
wakimkaba kwa nguvu beki wa Simba, Haruna Shamte (katikati) katika mechi
ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa jana Jumapili jijini Dar es Salaam.
By MWANDISHI WETU
(email the author)
- Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ashanti United pambano lake liliingiza Sh86,035,000 kutokana na watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza Sh53,815,000 kwa watazamaji 9,629.
Yanga iliyoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya
Ashanti United pambano lake liliingiza Sh86,035,000 kutokana na
watazamaji 14,261. Mechi ya Simba ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya
Rhino Rangers kutoka Tabora iliingiza Sh53,815,000 kwa watazamaji 9,629.
Mgawanyo kwa mechi ya Yanga ulikuwa Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) Sh13,123,983.05 gharama za kuchapa tiketi
Sh2,910,300 wakati kila klabu ilipata Sh 20,650,211.50.
Uwanja Sh10,500,107.54, gharama za mechi Sh
6,300,064.53, Bodi ya Ligi Sh6,300,064.53, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) Sh3,150,032.26 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) Sh2,450,025.09.
Mechi ya Simba mgawo ulikuwa Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) Sh8,209,067.80, gharama za kuchapa tiketi Sh2,910,300
wakati kila klabu ilipata Sh12,595,211.50. Uwanja Sh6,404,344.83,
gharama za mechi Sh 3,842,606.90, Bodi ya Ligi Sh3,842,606.90, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh1,921,303.45 na Chama cha Mpira wa
Miguu, Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh1,494,347.13.
0 comments:
Post a Comment