Tuesday, February 4, 2014

Man Utd wazidisha mazoezi Rooney aenda Marekani Van Persie bado majeruhi

                                            Van Persie na Wayne Rooney. 
  • Hata hivyo, itaendelea kukosa huduma ya mastraika wake makini, Wayne Rooney na Robin van Persie kwa kuwa bado hawapo fiti kutokana na kuuguza majeraha yao.

MANCHESTER, ENGLAND
WACHEZAJI wa Manchester United wamedhamiria kuachana na mwaka wa tabu! Sasa wameanza kukesha mazoezini ili warejee njia zao za ushindi na kuepuka msimu wa aibu.
Hata hivyo, itaendelea kukosa huduma ya mastraika wake makini, Wayne Rooney na Robin van Persie kwa kuwa bado hawapo fiti kutokana na kuugua.
Rooney amepelekwa Marekani kwenye hali ya hewa ya joto ili kufanya mazoezi ya kumaliza tatizo la majeruhi ya nyonga, wakati Van Persie bado hajapona maumivu ya paja.
Man United imepokea vipigo vitatu mfululizo kutoka kwa Tottenham katika mechi ya Ligi Kuu England, Swansea City katika mechi ya Kombe la FA  na Sunderland katika pambano la Kombe la Ligi, leo Jumamosi itacheza tena na Swansea uwanjani Old Trafford. Katika mechi hizo tatu imefungwa 2-1 kila mchezo.
Katika msimamo wa Ligi Kuu England, Manchester United ipo nafasi ya saba ikiwa imeachwa nyuma kwa pointi 11 na vinara Arsenal pia ipo katika hatihati ya kushindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Hata hivyo, sasa kipa namba moja wa timu hiyo, David de Gea, amedai wachezaji wa timu hiyo wamepagawa na vipigo hivyo na huwa wanabakia mazoezini kwa ajili ya kujifanyisha mazoezi ya ziada kuokoa msimu wao mbovu.
“Mara nyingi tunabaki mazoezini baada ya programu tukifanya mazoezi ya krosi na kumalizia. Tunafanya sana hasa wakati ambapo hakuna mechi katika siku zinazofuata nadhani inanisaidia mimi na wachezaji wengine kuimarika,” alisema kipa huyo.
Dea Gea ameongeza kuwa amekuwa akifanya mazoezi ya ziada mara kwa mara na mshambuliaji Javier Hernandez ‘Chicharito’ kwa ajili ya kuonyeshana ubabe na kuimarishana.
“Tunajaribu kusaidiana. Anajaribu kuniweka katika wakati mgumu na mimi namweka katika wakati mgumu. Siku zote tunajaribu kufanya kila tunaloweza na Chicharito ni mchezaji anayejituma kwa kila kitu mazoezini.
“Ni mmoja kati ya wachezaji wa ukweli wa kulipwa ambao nimewahi kuwaona katika maisha yangu ya soka. Ni mchezaji mahiri sana na rafiki bora pia.”
Kuhusu Rooney, ambaye awali alidai ana uhakika timu yao itarekebisha mambo licha ya vipigo vitatu mfululizo ataendelea kukosekana jambo linaloiweka timu hiyo kwenye wakati mgumu zaidi.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe