Tuesday, February 4, 2014

Mlela afurahi kuwa na mtoto

Mwigizaji nyota anayetamba na filamu yake mpya ya Nesi Selena, Yusuf Mlela 
Msanii huyo anasema kuwa awali baada ya kufungua kampuni yake kwa ajili ya utengenezaji wa filamu, alifurahi kupata furaha nyingine ya kuwa na mtoto kitu ambacho kwake ni hatua kubwa ya kusonga mbele katika kujijengea familia.
MWIGIZAJI nyota anayetamba na filamu yake mpya ya Nesi Selena, Yusuf Mlela, anafurahia maisha yake mapya na mwanaye aliyezaliwa mwaka jana.
Anasema maisha yake yamebadilika kwa kuwa karibu na mwanaye huyo, Mwantumu.
“Siku hizi hata ratiba zangu zinakuwa tofauti kwani lazima nipange muda pia kwa ajili ya baby, ni jambo ambalo linanifurahisha kuwa na mtoto. Ninapenda kujenga mapenzi mema na mtoto, hasa kuwa karibu na Mwantumu,” alisema.
Msanii huyo anasema kuwa awali baada ya kufungua kampuni yake kwa ajili ya utengenezaji wa filamu, alifurahi kupata furaha nyingine ya kuwa na mtoto kitu ambacho kwake ni hatua kubwa ya kusonga mbele katika kujijengea familia.

0 comments:

Post a Comment

Designed by Adamu Mwanakatwe