Waafrika vijana watakaong’ara Kombe la Dunia 2014
Huyu ni miongoni mwa waafrika watakaong'ara kombe la dunia 2014
Katika Fainali za Kombe la Dunia 2014, bara la Afrika
litawakilishwa na nchi tano ambazo ni Nigeria, Ghana, Cameroon, Algeria
na Ivory Coast.
Nchi hizo zote tano zina wachezaji wengi nyota
wanaocheza katika Ligi Kuu za nchi mbalimbali barani Ulaya, ambapo
wachezaji hao wapo walio na chini ya miaka 22 na wengine ni zaidi ya
miaka 22.
Spoti Mikiki inaangalia baadhi ya nyota wa Afrika
wenye umri chini ya miaka 22 watakaokuwapo katika Fainali za Kombe la
Dunia 2014 na wanatarajiwa kufanya vyema katika fainali hizo, wafuatao
ni wachezaji hao:
Ahmed Musa
Ingawa ana miaka 21, Ahmed Musa tayari ni mchezaji
muhimu katika klabu yake ya CKSA Moscow ambayo ameichezea mechi nyingi
za Ligi Kuu na kimataifa. Mwanzoni mwa mwaka jana akiwa na kikosi cha
timu yake ya taifa ya Nigeria alicheza mechi zote hadi timu hiyo
ilipotwaa ubingwa wa Afrika.Pia mwaka jana akiwa na klabu yake ya CKSA
Moscow alitwaa ubingwa wa Russia
Kijana huyu anatarajiwa kung’ara katika Fainali za
Kombe la Dunia mwaka huu kutoka na kasi aliyonayo uwanjani na akili ya
mchezo wa soka aliyonayo.
Christian Atsu
Atsu (22) amekuwa akipata wakati mgumu wa kupata
namba ya kuanza katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana chenye
wachezaji wengi nyota wanaocheza soka katika Ligi Kuu mbalimbali barani
Ulaya.
Hata hivyo Atsu amekuwa akikibadilisha kikosi cha Ghana kila anapoingia katika kipindi cha pili akitokea benchi.
Hivyo katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu
anatarajiwa kufanya vizuri akiwa bado ana umri mdogo. Mwaka jana Atsu
alisajiliwa na klabu ya Chelsea ya England kwa mkataba wa miaka mitano
na baada ya hapo ilimtoa kwa mkopo katika klabu ya Vitesse ya Uholanzi.
Fabrice Olinga
Wakati mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon
na klabu ya Chelsea, Samuel Eto’o akiwa anaelekea kustaafu kucheza soka,
Cameroon hivi sasa inawandaa vijana wadogo wawili ambao wote wanacheza
soka katika Ligi Kuu ya Hispania. Wachezaji hao ni Fabrice Olinga na
Jean Marie Dongou.
0 comments:
Post a Comment