MPASUKO ZAIDI CHADEMA
- M/KITI SINGIDA AJIUZULU, ASEMA HAKUNA DEMOKRASIA
Damiano Mkumbo na Darlin Said
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Singida, Wilfred Kitundu,
amejiuzulu rasmi nafasi hiyo akipinga mambuzi ya Kamati Kuu kuwavua nyadhifa za uongozi viongozi wake watatu.
Viongozi hao ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Bw. Zitto Kabwe, Dkt. Kitila Mkumbo na Bw. Samson Mwigamba ambao wanadaiwa kukisaliti chama hicho.Akikzungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Kitundu alisema kinachoendelea ndani ya chama hicho kwa sasa ni udhalilishaji wa demokrasia ya kweli.
Alisema uamuzi aliochukua ni hiari yake bila kushawishiwa na mtu akiwa na dhamira ya kulinda demokrasia ya kweli ili
kuhakikisha inaimbwa na kutekelezwa kwa vitendo."Mimi ni mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA,
mkoani hapa pia ni mwanachama wa 300 kitaifa, ninayo heshima kubwa kwangu, sipo tayari kuipoteza heshima hiyo kwa
kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia.
"Nitaendelea kuwa mwaminifu na mwadilifu ili kutetea
haki na Demokrasia siku zote bila kurudi nyuma," alisema na
kuongeza kuwa, kitendo cha kumvua nyadhifa za uongozi Bw. Kabwe na
wenzake si kizuri na kimeacha maswali mengi yanayoulizwa na wanachama wake," alisema Kitundu.
Aliongeza kuwa, msimamo wa CHADEMA mkoani humo ni kulaani, kupinga na kukemea maamuzi hayo ambayo yamejaa chuki, hofu na wasi wasi mwingi hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ndani ya chama.
Katika barua yake ya kujiuzulu ambayo alimwandikia Katibu Mkuu wa chama hicho mkoani humo, alisema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Bw. Freeman Mbowe, anapaswa kutoa neno ili wanachama na wananchi waendelee kikielewa vizuri chama hicho badala ya kikigawa vipande.
"Msimamo mwingine ni kumtaka Bw. Mbowe na Katibu Mkuu,Dkt. Wilbrod Slaa, kuitisha mara moja mkutano wa Baraza Kuu la chama ili kutoa maamuzi ya suala hili kwani lilifanywa na
watu wachache kwa masilahi yao," alisema.
Alishauri jambo hilo ni la
msingi sana na
maamuzi ambayo yatatolewa yame makini ili kudumisha hali ya utulivu ndani ya chama kiendeleze umarufu wake kwani ipo siku kinaweza kuongoza dola.Kitundu mbali ya kushika nafasi ya Mwenyekiti wa chama
Mkoa, pia aliwahi kuwa muasisi na mlezi wa CHADEMA
(1992-2013), Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa (1992-2013) na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (1992-2013).
Katika hatua nyingine, Katibu wa CHADEMA mkoani humo,Bw. Patric Msuta, amekiomba chama hicho kuitisha kikao cha Kamati Kuu kikae meza moja na viongozi wenye mgogoro na chama ili kumaliza tofauti zilizojitokeza.
Bw. Msuta aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano wake waandishi wa habari na kusisitiza kuwa, tangu mgogoro huo uanze, hakuna mwanachama aliyerudisha kadi."Hapa Singida, chama chetu hakina mpasuko wowote kwani
wanaelewa vizuri msingi wa maamuzi wa Kamati Kuu kutokana
na mgogoro uliyopo ndani ya chama chetu ambao naamini
utamalizika kwa njia ya amani," alisema.
0 comments:
Post a Comment