LONDON, England MOJA ya sifa ya kocha Sir Alex Ferguson ni kutafuta
Big G kama waswahili tulivyozoea kuziita inakadiliwa kocha huyo
ameshatafuna maboksi 2,500 hadi sasa.
Idadi hiyo inakadiliwa kutokana uwezo wake wa kutafuna big g 120 katika michezo 60 anayokuwa amekaa kwenye benchi msimu mzima.
Uongozi
wa Manchester United katika kuthamini mchango wake hapo tayari
imetangaza dhamira ya kutengeneza mnara wa kumbukumbu ya miaka 26, na
mafanikio makubwa kutoka kwa kocha huyo raia wa Scotland.
Mnara
huo utazinduliwa mwezi huu wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Queens
Park Rangers, klabu ambayo kocha huyo aliiongoza United kuanza safari ya
mafanikio.
Takwimu muhimu za maisha ya Ferguson akiwa klabu
hiyo ya Old Traffrod zinaonyesha kuwa nusu ya wachezaji alio nao
kikosini mwake walikuwa hawajazaliwa wakati alipoanza safari ile.
Hao
ni pamoja na kipa David De Gea, mabeki Rafael, Jonny Evans, Phil Jones,
Chris Smalling, viungo Anderson, Nick Powell, Tom Cleverley, Shinji
Kagawa,washambuliaji Danny Welbeck na Javier Hernandez, ambao kwa sasa
ni baadhi ya nyota ambao wanacheza kikosi cha kwanza cha Man United.
Hakuna
shaka kwamba Ferguson amekuwa kocha mwenye mafanikio makubwa ambayo ni
vigumu kwa wengi kuyafikia. Amebuni mbinu na kuzitumia kujenga kikosi
imara cha muda mrefu.
Nyota ambao Fergie aliwahi kuwa nao, kisha kuwatimua Kocha
huyo ambaye anatimiza miaka 71 siku ya mwaka mpya, bado anaonekana
kama mtu anayeweza kudumu kwa miaka mingine kumi ijayo. Umri wake
unamfanya aonekane kama kocha ambaye ni vigumu kufahamu ni lini
atatundika daluga na kuiacha United. Unaweza kujiuliza, ni lini
Ferguson anapofikiria kungíatuka? Jibu linapatikana katika kikosi chake
ambacho anakijenga msimu huu licha ya kukabiliwa na tatizo katika
ulinzi, ingawa amefanikiwa kuiweka United kileleni mwa Ligi Kuu, pia
ikiongoza kundi lake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ingawa
ana uchungu wa kushindwa kutetea taji msimu uliopita, Ferguson anaeleza
kuwa hilo lilitosha kumpa fundisho baada ya wapinzani na jirani zao,
Manchester City kutwaa ubingwa kwa tofauti ya mabao. Hilo limemtosha
Ferguson kufikiria mbinu za kuipa United ubingwa msmu huu na kufikia
kilele cha mafanikio katika soka ya England.
Licha ya mafanikio
makubwa ambayo yamempa mataji 37, wazo kuu la uongozi wake akiwa Old
Trafford ni mtazamo wake wa kusaka mafanikio, akiwataka wachezaji wake
kusahau yaliyopita na kufikiria mbele waendako . Huo, ndio umekuwa
msimamo wa kocha huyo akiwa United , akiweka kando ndoto za uzee na
kufikiria jinsi ya kuipa mafanikio zaidi klabu yake, akieleza kuwa
sikuzote hafikirii maisha baada ya kungíatuka soka. Mara kadhaa, Ferguson ametangaza kustaafu, lakini akababili mtazamo na mawazo yake na kuendelea kusaka mafanikio akiwa United.
Mashabiki
wengi wa United wamekuwa wakijiuliza ni lini litatokea katika maisha
ya klabu yao baada ya safari ya Fergie, ingawa yeye binafsi ameweka
kando fikra hizo na hata warithi ambao wamekuwa wakitangazwa kuchukua
mikoba yake kama vile, Sven Goran Eriksson, kocha aliyewahi kuinoa timu
ya taifa ya England.
Mwaka 2002, kocha huyo alitangaza kustaafu,
lakini ghafla akabadili mawazo na kubakia kwa miaka kumi mingine yenye
mafanikio na kutwaa mataji matano ya ligi, moja la Ulaya, jingine la
Kombe la FA, matatu ya Kombe la Ligi na moja zaidi la klabu bingwa ya
dunia.
Kipindi aliposherehekea robo karne ya uongozi wake akiwa
United msimu uliopita, Ferguson alijibu swali la lini anafikiria
kungíatuka kwa kueleza, ìNina miaka miwili au mitatuî zaidi klabuni
hapa.
Baada ya kosa la awali la kutangaza kungíatuka kwake,
Ferguson aliapa kutorudia tena kosa hilo, jambo ambalo limefanya siri ya
lini ataiacha klabu hiyo.
Kwa kutambua ugumu wa kazi ile akiwa
United na aina ya kocha ambaye anafaa kwa kazi ile, mara kadhaa Fergie
amesema yeye si mtu wa kupendekeza nani wa kumrithi, ingawa anadhani
kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho au Pep Guardiola aliyekuwa
Barcelona wanafaa.
Mourinho, amekuwa na uhusiano mzuri na
Ferguson licha ya upinzani wao kwa ngazi za klabu, zama zile akiwa
Chelsea, bila shaka raia huyo wa ureno anao wasifu ( CV) na mapafu ya
kuinoa United baada ya Ferguson kuondoka.
Kocha huyo ametwaa
mataji akiwa England, Italia, Ureno na sasa Hispania akiwa na Real
Madrid, mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Porto (Ureno),
Inter Milan, Italia, yameboresha wasifu wake kama mrithi anayefaa kwa
Ferguson.
Kwa sasa, Real Mardid inacheza aina ya soka ya kipekee
ambayo haifanini na ile ya Mourinho akiwa Porto, Chelsea na Inter,
jambo ambalo linatia hofu mashabiki wa United endapo ataitwa kwa kazi
ya kuinoa United.
Guardiola, kwa upande wake ambaye aliijenga
Barcleona , kikosi ambacho Ferguson alikiri kwamba ni bora duniani,
baada ya kuwashinda katika fainali mbili za 2009, 2011, pia anapigiwa
upatu.
Ferguson na Guardiola, ambaye hana kazi kwa sasa walikutana
New York tangu Septemba wakati ule Fergie akimshangilia mchezaji tenisi
raia wa Scotland,Andy Murray kwenye michuano ya US Open, ambayo
alishinda.
Ni wazi kwamba Guardiola anabaki mmoja wa watu ambao
wanapewa nafasi ya kuvaa viatu vya Fergie na kama kocha huyo atapewa
nafasi ya kuteua mrithi.
Sir Alex Ferguson na Pep Guardiola... je, ndiyo mrithi wake?
Ferguson anawaona Mourinho na Guardiola, kama vijana wawili makini, ambao angependa kuona mmoja wao akirithi mikoba yake.
Ni
dhahiri kwamba Fergie angependa kusherehekea miaka 26 akiwa United kwa
kutangazwa kocha bora wa mwezi Oktoba, ikiwa ni mara ya 27 kwake.
Mnara
ambao unajengwa nje ya Uwanja wa Old Traffrrod katika eneo lijulikanalo
kama Sir Alex Ferguson Stand, jukwaa ambalo awali liliitwa North Stand,
utasimikwa Novemba 23.
Takwimu muhimu za miaka 26 ya Fergie akiwa United
37- Mataji makubwa jumla
12- Mataji ya Ligi Kuu
5- Makombe ya FA
4- Makombe ya Ligi
2- Makombe ya Ulaya
1,461- Mechi alizosimamia United
871- Mechi alizoshinda
260- Mechi alizofungwa
330 ñ Mechi alizotoa sare
2,693- Mabao yote
1,323- Mabao waliyofungwa United
1,988- Pointi za Ligi Kuu
213- Dakika ambazo United imesubiri kufunga bao la kwanza chini ya Ferguson, ushindi wa 1-0 dhidi ya QPR, November 22, 1986
185 ñ Idadi ya wachezaji aliosajili United
45- Rekodi ya mechi ambazo United haikufungwa
9-0 ñ Ushindi mnono wa United dhidi ya Ipswich, Old Trafford mwaka 1995
6-1 ñ Kipigo kikubwa cha United dhidi ya Manchester City mwaka 2011
Pauni 30.75m ambazo alilipa kumsajili Dimitar Berbatov mwaka 2008 kwa Spurs
Pauni 80m- Fedha zilizopatikana kwa mauzo ya Cristiano Ronaldo kwenda Real Madrid, 2009
14- Namba ya makocha ambao Man City imekuwa nao wakati Ferguson akiwa United.
17- Mechi ambazo alizikosa kwa kutumikia adhabu
2,500- Boksi za vitafunwa Big G (chewing gum) ambazo ametafuna Ferguson wakati wa mechi za United.
0 comments:
Post a Comment