Msigwa asomewa mashtaka kwa tuhuma za kujeruhi
Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini, Mch. Peter Msigwa amefikishwa
katika mahakama ya wilaya ya Iringa muda mfupi uliopita akidaiwa
kuhusika na uchochezi na kusababisha vurugu katika kampeni za udiwani
Kata ya Nduli.
Mch. Msigwa alikamatwa jana jioni baada ya kutokea kwa vurugu hizo katika mkutano wa kampeni wa chama cha Chadema.
Mwandishi wetu aliyepo mahakamani hapo anasema
hali ya ulinzi imeimarishwa huku kukiwa na idadi kubwa ya wafuasi wa
Chadema, ambao hata hivyo wamesimama mbali na eneo la mahakama huku eneo
hilo likilindwa na askari wa kutuliza ghasia (FFU).
Baada ya kusomewa mashtaka yake amekana na ameachiwa huru kwa dhamana, kesi hiyo itatajwa tena Machi 10 mwaka huu
Mbunge wa Chadema kortin vurugu za kampeni
Shija Felician, Mwananchi
Kahama. Mbunge wa Jimbo la Maswa
Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya
Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani
kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za
uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao
wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00
mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi
Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha
Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda
makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao
wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa
mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za
kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya
Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi
kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo
washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba
mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao
wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
0 comments:
Post a Comment