KUTOKA LONDON: Ligi Kuu England imefika pagumu
Ligi Kuu England (EPL) imefika katika mzunguko wa 25 na kwa kweli ni pagumu.
Ni vigumu kutabiri timu gani itachukua ubingwa pia zipi zitashuka daraja. Hii ni kutokana na matokeo yanavyochanganya.
Manchester City iliyosifika kwa upachikaji wa
mabao mengi kuliko timu nyingine, imekumbwa na hofu kutokana na matokeo
ya mechi zake mbili zilizopita.
Kufungwa na Chelsea nyumbani ikiwa ndio mechi ya
kwanza waliyopoteza Etihad tangu kuanza msimu huu na kwenda suluhu na
timu dhaifu ya Norwich City, kunaacha maswali mengi.
Vijana hao wa Manuel Pellegrini, wapo nafasi ya
tatu katika msimamo wa ligi hiyo huku wakiwa bado na mechi ngumu ugenini
na inatabiriwa kwamba wanaweza kudhoofishwa zaidi.
Kocha Jose Mourinho ‘The Happy One’ wa Chelsea kudai kwamba timu yake haipo kwenye mbio za ubingwa, inaonekana kama utani.
The Blues wameimarika sana na mfululizo wao wa ushindi umewaweka pazuri, wakiongoza ligi sasa halafu wakiwa wanajiamini zaidi.
Arsenal iliyokuwa inaongoza ligi kwa muda mrefu na
tena kwa tofauti kubwa ya pointi, imeanza kunyong’onyea. Ilitoka sare
na timu isiyotarajiwa na kisha kuja kubugizwa mabao 5-1 na Liverpool.
The Gunners na Manchester City zinaweza kujitetea
kwamba hali yao inasababishwa na wachezaji wao muhimu kuwa majeruhi,
lakini walikuwa na nafasi na walisajili wachezaji wengi.
Kwa Sergio Agueri kukosekana Manchester City na Theo Walcott kuwa majeruhi Arsenal, hakumaanishi kwamba hakuna wengine.
Lakini inavyoelekea ni kwamba athari za kukosekana
kwao ni kubwa ijapokuwa bado wana nafasi nzuri ya kuliendea taji la
ligi hii maarufu zaidi duniani.
Timu hizo zinapishana kwa pointi moja moja tu,
Chelsea wakiwa juu wakifuatiwa na Arsenal na Manchester City huku
Liverpool ikija kwa mbali kidogo.
RSS Feed
Twitter
9:54 PM
Unknown
0 comments:
Post a Comment