
KOCHA Mwingereza, Dylan Kerr, alipewa mkataba na Simba mwishoni
mwa Juni. Baada ya kama wiki hivi akaenda mazoezini pale Chang’ombe.
Alipofika kitu cha kwanza kilichomshtukiza ni aina ya uwanja aliokuta
wachezaji wanafanyia mazoezi. Lakini baadaye akakausha.
Akatumia kama siku tatu hivi kusoma wachezaji
lakini ndani ya huo muda uso wake ukaonyesha anatafakari sana.
Akawaambia viongozi timu iende Tanga apate muda wa kuwasoma jamaa
vizuri. Viongozi wakamuuliza unaonaje mziki wetu? Akajifanya kama
hajasikia akawaambia kaeni hapo niwaambie kitu.
Wakamtajia makipa akawaambia nataka mniongezee
mmoja, wakaingia kwenye beki akasema anataka pia mpya mmoja, kiungo
akakuna kichwa kidogo akawaambia wamuongezee pia mmoja. Ilipofika kwenye
mastraika sasa akawambia acheni masihara inabidi tuingie mfukoni
tusajili.
Jamaa mmoja akamwambia hata yule (anamtaja) na
...(anamtaja pia ) ina maana hawafai? Mzungu akamwambia mimi ndiye kocha
nataka straika. Baada ya mechi na SC Villa mzungu akamuita chobisi
kiongozi mmoja akamwambia umeona nlichokwa namaanisha? Nafasi 14
unafungaje bao moja? Jamaa akasema ni kweli aisee ngoja tukajipange.
Simba ikafanya mishemishe na kuwaleta nchini
straika Mrundi Kevin Ndayisenga na Makan Dembele raia wa Mali ambao
walianza mazoezi na timu hiyo jana Jumatano.
Dembele aliwahi kutamba na Raja Cassablanca ya
Morocco miaka ya nyuma na taarifa kutoka katika mitandao zinaonyesha
kuwa mara ya mwisho aliichezea JS Kabylie ya Algeria mwaka 2013.
Ndayisega anatokea Atletico ya Burundi.
Kerr ameomba kuwaona mastraika hao wawili katika
mazoezi yake kwanza kabla ya kuwapa ruhusa viongozi kukamilisha usajili
wao kutokana na kuwepo kwa wasiwasi wa kusajili mastraika wa viwango vya
kawaida.
“Nimewaomba viongozi wasifanye usajili kwanza,
walete wachezaji tuwaone na hata hao wawili inabidi nijiridhishe na
uwezo wao kwanza, tunahitaji mtu makini katika ufungaji,” alisema Kerr
ambaye amemkataa Elius Maguli na kuwaambia viongozi wampeleke kwa mkopo
popote ingawa baadhi yao bado hawaamini uamuzi huo.
Rais wa Simba, Evans Aveva alikiri kuwa bado wana
kazi kubwa ya kukamilisha usajili huo wa straika lakini kocha ndiye
mwenye uamuzi wa mwisho baada ya kuwaona wale watakaofanya majaribio.
“Lengo letu kubwa ilikuwa kwa Mavugo lakini dili
likakwama, sasa tumemwachia kocha atoe uamuzi juu ya hawa waliopo, ni
kweli timu inahitaji straika,” alisema Aveva ambaye ameasisi mauzo ya
jezi halali za Simba ambapo moja huuzwa 15,000.
Simba inaumiza kichwa kwa sasa kupata straika
makini atakayeweza kuzitumia vizuri nafasi zinazotengenezwa na timu hiyo
baada ya mastraika waliopo kushindwa kumvutia vilivyo Kerr.
Awali timu hiyo ilifanya mazungumzo na straika wa
Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo ambaye alikubali kutua Msimbazi kabla
ya baadaye kuzuiwa na rais wa timu
0 comments:
Post a Comment