
KARIBUNI kwa
mara nyingine katika safu yetu maridhawa ya All About Love. Kwa mtu
anayejali, lazima atakuwa akipata vitu vinavyoweza kumsaidia katika
maisha yake ya kimapenzi anayoishi.Tunajua changamoto nyingi zilizopo
katika mambo yetu haya ya uhusiano.

Watu wanamwagiana maji ya moto, tindikali, kuchomwa visu na hata kuuana
kwa sababu ya mapenzi. Na usije ukadhani wanaofanyiana hivi ni wale
waliochepuka, hapana, wakati mwingine mume anamfanyia hivyo mke wake au
mke anamfanyia mume wake.
Na kinachosababisha litokee hivi, siyo mara zote linahusiana na mapenzi
moja kwa moja, ni kitu kingine kabisa. Maana tumezoea mume au mke
kumfanyia mwenzake unyama kwa sababu labda alimfumania na mtu mwingine.
Hii inatokana na jinsi tusivyo huru kimawazo katika kukabiliana na
changamoto zinazokuja mbele yetu. Kuna kitu kimoja ambacho wanandoa
wengi na walio katika uhusiano wanashindwa kukielewa kuwa ni cha msingi
sana katika maisha yao ya kimapenzi.
Kauli
Kauli ni jambo linaloonekana dogo, lakini lina madhara makubwa sana, siyo tu katika mapenzi, bali hata katika maisha ya kawaida tunayoishi uswahilini. Ndiyo maana unaweza kuwa umeshasikia mara nyingi sana habari kuwa mtu kachomwa kisu kwa deni la shilingi mia moja au hata elfu moja.
Kauli ni jambo linaloonekana dogo, lakini lina madhara makubwa sana, siyo tu katika mapenzi, bali hata katika maisha ya kawaida tunayoishi uswahilini. Ndiyo maana unaweza kuwa umeshasikia mara nyingi sana habari kuwa mtu kachomwa kisu kwa deni la shilingi mia moja au hata elfu moja.
Unajiuliza mara nyingi ni vipi umuue mwenzako kwa deni dogo kiasi hiki,
lakini kumbe nyuma ya pazia ni kauli. Badala ya mdaiwa kutoa majibu
mazuri, anajibu ovyo, mtu anapandisha hasira, ibilisi anafanya kazi.

Katika nyakati mbaya za uhusiano wenu, kauli ndicho kitu pekee
kitakachoweza kuboresha palipoharibika au kuharibu kabisa. Unaweza
kuzungumza na kutuma ujumbe ukafika bila kutoa mapovu.
Unapotaka kukabiliana na mwenza wako, ili uende sawa ni lazima kwanza
upunguze hasira, ujiweke katika nafasi ambayo unaweza ukazungumza na
mwenzako akakuelewa. Tunachokosea sisi, tunatanguliza hasira na kauli
zisizofaa, ndiyo maana moto unazidi kuwaka.
Kwa mfano, umekuta mipira ya kiume katika mfuko wa suruali ya mpenzi
wako. Ni dhahiri kwamba hiyo si kwa ajili yako. Kama ni matumizi
atatumia na mwanamke mwingine. Ingawa hiyo ni dalili iliyo wazi kabisa
kuwa mwenzako ni mchepukaji, lakini haikufanyi kuwa na hasira na kuondoa
staha katika kumkabili.
Kwanza mshukuru Mungu kwamba angalau mwenzako anajali. Hawezi kukuletea
maradhi kutoka huko kwenye michepuko yake. Lakini pia, ukimuendea
taratibu, aibu ya kibinadamu itamshika, hata kama hatasema, lakini
atajutia.
Kauli ya ukali kwa jambo kama hili, unaweza kumpa nafasi ya kukugeuzia
kibao. Nikuambie kitu, siku zote watu wakosefu hutafuta udhaifu wa
anayemhusu katika kukabiliana naye. Kama unafoka, anaweza kuondoka
nyumbani akijidai unampigia kelele na pengine akaenda kufanya kweli
kabisa, ili kukukomoa!
Ikitokea hivyo, utakuwa umekosa kujua sababu ya yeye kuja na kondom
nyumbani, ungekwenda taratibu, ungemnyima nafasi ya kuongopa, badala
yake angekuomba msamaha. Kumbuka, KAULI NI SILAHA YAKO NAMBARI ONE!
0 comments:
Post a Comment