Dhumuni la kukukumbuka leo si lingine bali ni kuhusu ishu ya usagaji. Siku hizi wimbo wa usagaji kwa mastaa umekuwa kama wa taifa.Nimekuwa nikisikia matukio kadha wa kadha ya kisagaji kwa mastaa kitu ambacho naamini tusipokemea, vizazi vyetu vitazidi kuangamia.
Kupitia kazi yangu ya uandishi, mara nyingi nimekuwa nikikutana na wewe katika matukio mbalimbali. Naamini yapo ambayo yanakuwa na ukweli, yapo ambayo pia huwa unazushiwa.Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo? Malizia mwenyewe. Hata katika yale matukio wanayokutajataja, hawakutaji hivihivi kuna viashiria wameviona ndiyo maana wamekuwa wakikutaja.
Nisiku hukumu lakini kuna kitu cha kujifunza katika eneo hilo. Nimeshafanya uchunguzi mdogo na kugundua kuwa wengi wanaofanya michezo ya aina hiyo, wanakuwa na sababu lukuki.Wapo ambao hawaridhishwi na wanaume, wengine wanafanya hivyo kama njia ya kukwepa maradhi na wengine ni kwa sababu ya urahisi wa kujistarehesha eti kwa kuwa mwanamke mwenzake ni rahisi kumpata kuliko mwanaume ambaye mara nyingi anajifanya yupo bize.
Nikukumbushe kwamba desturi zetu kama Watanzania hivyo vitendo vya penzi la jinsi moja havikubaliki. Vipo vitu vya kuiga kutoka katika tamaduni mbalimbali lakini binafsi naona kama hicho hakifai.Hata tendo la ndoa ambalo limehalalishwa katika vitabu vya dini ni lile la mke na mume. Hivi vitu vya kuiga kidogo inabidi viwe na mipaka, si kila king’aacho ni dhahabu.
Juzikati kupitia moja ya magazeti Pendwa, SMS zako zilizokuwa zikifanya makubaliano ya kuashiria upo tayari kusagana na binti mdogo zilinaswa live na mapaparazi.
Mbona starehe zipo nyingi sana dada yangu, wanaume pia mbona wapo wa kumwaga. Unataka kuniambia katika wanaume wote uliowahi na ambao unao sasa hawakupi ile kitu roho inapenda?
Wewe ni kioo cha jamii, watu wanategemea vitu vingi vya kujifunza kutoka kwako.
Nikukumbushe tu kwamba, una kundi la watu ambalo lipo nyuma yako tangu ulipokuwa mtangazaji hadi ulipoangukia katika anga la filamu.Wote hao wanategemea uwe na mwisho mwema ili waweze kukukumbuka maishani. Wajifunze kupitia njia zako ili pengine na wao wawe kama wewe au zaidi yako.
Naamini umenielewa, kiroho safi kabisa nakuomba ubadilike. Sitegemei kukuona ukitajwatajwa katika michezo michafu kama hiyo kwani inakushushia heshima na hadhi yako ambayo umeitengeneza kwa muda mrefu katika jamii. Kwa leo naweka nukta hapo, Mungu akusimamie!
0 comments:
Post a Comment